Thursday, January 30, 2014
SHETANI ALINIFANYA NITOKWE NA HAJA KUBWA BILA KUJITAMBUA
Ndugu wapendwa tunaishi katika dunia iliyojaa kila aina maovu na uonevu mwingi sana.
wakati mwingine tunatafuta msaada kwa wanadamu lakini msaada wa wanadamu ni wa muda tu na uongo ni mwingi sana.
Naitwa John niko Arusha na ni mwenyeji wa hapa hapa Ungalimited Arusha.
nina miaka 31 na nimeoa na kujaaliwa kupata mtoto mmoja pia nimeokoka tangu 2010.
katika maisha yangu ya nyuma kabla ya wokovu niliteswa sana na nguvu za giza na ilifika kipindi cha kukata tamaa yapo memgi sana yaliyonitokea lakini hili la kulala na paka hua mpaka sasa nikikumbuka nasisimka nywele japokua nafahamu kwa sasa siwezi kuchezewa na uchawi tena maana YESU niliyenaye amenishindia na atanishindia milele.
Ilikua nov 2008 ilikua siku ya jumatano nilienda kuangalia mpira UEFA na nilirudi mida ya saa 5 usiku na nilipofika nilipokua nimepanga niliingia ndani na kuwasha taa
hakukuwa na kitu na baadae nikafunga net na kulala ilipofika saa 10 alifajiri nilijikuta nasikia joto maeneo ya kifuani na kuanza kupapasa labda ni mto wa kuegemea kichwa ulikua umekaa pale na nilipoanza kupapasa niligusa manyoya na nilipozidi kupapasa nilizidi kugusa manyoya kitendo kilichosababisha kuamka kwa nguvu na kutoka ndani ya chandarua haraka huku nikiogopa sana .
nilipotoka niliwasha taa na kumwona paka mkubwa sana mweusi ambaye hata sijui ameingiaje chumbani kwangu maana hakuna sehemu ya kupitia paka kama huyo
pili ameingiaje ndani ya kitanda maana kuna net nafunga yaani hata iweje paka kama huyo katika mazingira ya kawaidi hawezi kuingia kwenye chandarua
tatu ameingiaje kwenye shuka na kulala tena kujinyoosha kama binadamu
nne kajifunika shuka langu je ana akili za kuchukua shuka na kujifunika?.
Haikua kawaida ni nguvu za giza sasa nikaanza kuwaza kwamba ni nani anayenichezea hivyo na nilitafakari ni nani ni adui yangu au ni nani tumekosana siku za karibuni hata akaanza kunifanyia hivyo?
Nilifungua mlango na kutoka nje maana yule paka duh niliogopa hata kumfukuza maana ni mkubwa na anatisha yaani ukubwa wake ni kama chui saizi ya kati.
nilizunguka nyuma na kuanza kuchungulia dirishani na baada ya kama dakika 8 yule paka aligeuka na kuwa nyoka na baada ya muda kidogo yule nyoka akawa anatoa mwanga japokua taa ilikua inawaka lakini yeye alitoa mwanga kama wa moto na baada ya muda kidogo akatoweka.
Sikuingia ndani ya chumba changu hata saa 6 mchana na kwa tukio hilo la siku moja nilijikuta nawachukia watu sana na kuanzia muda huo moyoni mwangu kila mpangaji mwenzangu nilimchukia na nakumbuka kulipokucha nikiwa nimejiinamia nje kwa kuogopa kuingia ndani kuna mama wa jirani alipita na kunisalimia kwa nia nzuri tu lakini kwa sababu ya taharuki moyoni mwangu nilimjibu kwamba nitamkatakata kwa mapanga kwa tabia yake ya uchawi.
yule mama alikodoa macho na kunishangaa na kusema uchawi upi tena?
akasema yeye hahusiki na uchawi na hawezi kuroga maana mambo hayo hayajui hata kidogo tena akasema nimwombe msamaha nilikataa maana nilihisi kwamba kihelehele chake cha kunisalimia wa kwanza ndicho kilichosababisha nimwambie vile kumbe ni kiwewe tu cha tukio la jana sikukaa kwa amani hata kidogo maana nilishuhudia kwa macho yangu jinsi paka alivyogeuka nyoka na kwa wiki nzima sikulala kwa amani na muda mwingi nililala mchana tena kwenye chumba cha rafiki yangu ambaye nilikua naenda kumtembela au kupiga story na nikifika tunaongea kidogo harafu nalala na kuna siku aliniuliza je usiku nalala wapi nikicheka tu na kumwambia nilikua nalala kwa girlfriend wangu kumbe haikua kweli.
baada ya wiki mbili nilianza kurudi kwenye hali ya kawaida na kuanza kulala maghetoni kwangu kama kawaida na hakukua na tatizo lile tena lakini baada kama ya mwezi mmoja kupita na nakumbuka siku hiyo ilikua siku ya jumamosi ni siku ambayo sitaisahau na ndio chanzo cha kukuandikia habari hii nililala na ilipofika kama saa 8 usiku nilijigeuza katika hali ya usingizi na kugusana na kitu kiguma kilefu kama binadamu tena kizima maana joto kama la mtu nililisikia.
nikaruka ghafla hadi net ikakatika nikakimbila mlango ili nitoke nje lakini niliukosa na kiukweli siku hiyo nilijinyea kabisa na hata sikujuia kinyesi kilitoka vipi lakini nilikuja tu kukuta nina mavi kuanzia kiunoni hadi miguuni na kilichoendelea baada ya hapo kuna kama mtu alinyanyuka kitandani na kuja kuwasha taa mawazo yangu yote nilimwazia paka wa siku ile. Baada ya kuwashwa kwa taa nilimwona msichana ambaye aliniambia kuwa siwezi kumkimbia hata siku moja aliniambia haraka nirudi kitandani na kulala maana hakujakucha.
kwa leo ni kama inachekesha lakini siku hiyo ilikua ni hatari kuliko hatari zote maishani mwangu nilirudi kitandani na yule dada aliyekua amevaa kimini aliniambia kwamba nilale na kuniambia tena kwamba tungefanya mapenzi ila mimi ni mchafu ninanuka mavi.
sikujibu neno hata moja maana kwa muda huo nilihisi kufakufa.
sikusinzia na yeye alikaa kwenye kiti na baada ya muda kidogo nilisikia kicheko na nlipochungulia niliona paka wa siku ile yaani yule binti wa kimini kageuka paka niliruka tena hadi chini na yule paka akaanza kuongea kama mwanadamu huku akinitukana kwamba nanuka sana kwa uchafu wa kinyesi na baada ya hapo alisema atakua anakuja kunitembelea maana amenipenda tena kwa miaka iliyo pita 10.
Sikujibu kitu na muda kidogo aligeuka na kuwa binadamu tena na akatoweka ghafla.
Sasa nilijua kilichokua kinaendela na kesho yake bila kuaga niliondoka na kuelekea singida nikiwa nimepanda basi la kuelekea mwanza tulifika salama na nikaenda kulala kulala gest pale singida na lengo langu kesho yake nitafute makao mapya maana nilikua na pesa kidogo kama laki 9.
***************************
Nikiwa nimelala usiku yule dada alinitokea tena na kuniambia kua siwezi kunikimbia hata siku moja na kwa taarifa yako ni kwamba tumesafiri wote ndani ya basi tena alikua amekaa jirani na mimi ila hakujionyesha kwangu ili nisishtuke na kujinyea mbele za watu.
sikujibu neno lolote na napenda kukuambia mtumishi kuwa baada ya pale yaliendelea matukio mengi tu na nikakimbilia Dar lakini ndio kwanza yule dada aliendelea kunisumbua na umbo lake la paka lakini mambo hayo ndio yakawa chanzo cha mimi kuokoka na tangu siku nimeombewa na kumkiri YESU KRISTO kuwa ni BWANA na MWOKOZI wa maisha yangu mwaka 2010
mambo haya hayajatokea tena na siku naombewa pale Sinza ilisikika tu sauti ya yule dada akisema ipo siku tu ataninasa na kuniua maana yeye na ndugu zake wameungua na moto m-baya uliotoka hapo kanisani.
Hawezi tena milele na hua najiuliza ilikuaje hata kuanza kunisumbua mimi na ilikaribia mimi kujeruhi watu kisa hili lii mzimu tena muda mwingine akiongea kwa kejeli na kicheko huku akinicheka kwamba nitajinyea?.
Hata hivyo kuna baraka katika KRISTO maana mwaka 2011 mwishoni nilifunga ndoa kule kule arusha ambako naishi sasa na tuna mtoto mwenye miezi 7.
Namshukuru sana MUNGU na hakika katika YESU tunaushindi na zaidi ya kushinda,
CHANZO: UKURASA WA FLORA MBASHA FACEBOOK
Wednesday, January 29, 2014
Majaribu hutoka kwa Mungu na Shetani?
Amani ya Bwana iwe pamoja enyi nyote.
Majadiliano na fafanuzi ktk mada hii bila shaka yatatusaidia na kutupa ufahamu tuepuke kuwanung’unikia na kuwalalamikia Mungu na Wanadamu. Neno ‘’Majaribu’’ linaeleweka na kutumiwa na wengi hata limetungiwa nyimbo za Injli lakini nilipotafakari kwa uangalifu mambo ya Mungu na tunavyolitumia neno ilo ktk maisha haya, nimelileta kama mada ili tupate ufahamu hasa kwenye swala la kufafanua ili kuweka utofauti wa wazi kipi ni hiki na wala si kile, kwa maana iyo kupitia ninyi vyombo vya kazi vya Bwana, tunaweza pata akili, uelewa, ufunuo, Neno, Maandiko, fundisho, uzoefu, ushuhuda nk kwa ajili ya kusaidiana na kujengana Kikanisa/Kiroho na Kiimani.
Ili kuuingia Mjadala vema, unaweza tafakari yasemwayo ktk Maandiko haya:
Kwa upande mmoja, Imeandikwa, furahini mnapoingia majaribuni-Yak.1:2, Wanafunzi walitishwa kutohubiri-Mdo.4:21,29,Stephano akapigwa mawe na kufa-Mdo.7:57-60, Mitume wanawekwa jela, wanapigwa na kuachiwa Mdo.5:16-42,Paul na Sila wakapigwa na kutupwa gerezani-Mdo.16:19-26,Petro anangojea kesho yake kuuawa baada ya mwenzake Yakobo kuchinjwa -Mdo.12:1-17, Ayubu anapoteza Watoto, Mali na Afya-Ayubu.1:14-19, 2:7, Mfalme Hezekia anaugua na Mungu anamwambia atakufa kisha akaomba, kifo kinafutwa-Isaya.38:1-4/ na 2Wafalme.20:1-4, Mtu ni kipofu toka kuzaliwa na ulemavu huo upo kwa ajili kazi za Mungu kudhihirishwa ndani yake-Yoh.9:1-5, Ainea ameugua na amepooza miaka 8 pia Dorcas mpendwa amekufa Petro anaomba, Ainea anapona na Dorcas anafufuka-Mdo.9:32-42, Mama Mkwe wa Petro amelala anaumwa homa, Yesu ana mgusa, anapona-Matt.8:14-15
Kwa upande mwingine, imeandikwa kuwa duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu-Yoh.16:33, Je tupate mema mkononi mwa Mungu nasi tusipate mabaya-Ayubu.2:10, jaribu halikuwapata ninyi isipokua lililo kawaida ya wanadamu-1Wakor.10:13.
Kutokana na kichwa cha mada, nakigawa kupata Maswali makuu 4 ili kutoa mwelekeo mzuri unapojadili/changia, nayo ni haya:
Moja: Tukio/jambo gani likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hili ni jaribu(test and trial, temptation)?
Mbili: Tukio/jambo gani likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hiki ni kitu cha kawaida tu kwa wanadamu kwakua wanaishi duniani na kwamba tukiomba au tusiombe, tuko kiroho sana au kidogo, tumeokoka au bado, lazima yatatokea/tupata tu bila shaka?
Tatu: Tukio/jambo gani likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hili ni jaribu(test and trial) toka kwa Mungu lenye nia ya kutuimarisha au hili ni jaribu(temptation) la shetani kututoa kwa Mungu?
Nne: Au kuweka katika uhalisia, Mfano Ukifiwa na Mke, Mme, Mtoto, gari ikiibiwa, pinduka, ukavunjika mguu, ukiibiwa mali dukani, ukavamiwa na majambazi, ukipigwa sokoni wakati una hubiri au umekaa tu bila kuhubiri, ukakabwa na vibaka, ukiugua ugonjwa, kanisa-jengo likiunguzwa, ukikosa kazi muda mrefu, ukipata kazi lakini bosi akawa mnyanyasaji, Kanisa kutokukua, huduma kudumaa, kutopandishwa cheo,kukosa pesa,kutoweza kujikimu kwa utele mahitaji ya maisha, kuchelewa kuoa/kuolewa, kutopata mtoto, kua tasa nk, yapi kati ya hayo ni majaribu toka kwa Mungu, Shetani au ni mambo ya asili au kawaida tu ktk maisha duniani hapa?
Press on,
Edwin Seleli
SOURCE: STRICTLY GOSPEL
Monday, January 27, 2014
RENEWING YOUR MARITAL RELATIONSHIP(2)
Dear Reader,
I welcome you to another edition of our series on Renewing Your Marital Relationship. Last week, you were told that one of the things to do to renew your marital relationship is having a right expectation. This week, by the enabling power of the Holy Spirit, we shall be examining how to Build A Strong Attitude of Intimacy.
Intimacy is the pillar for every successful marriage. It is the responsibility of the man and his wife to build and develop a strong and healthy intimacy in their marriage. Many couples wistfully remember those sweet, innocent times before marriage, that they were so interested in each other. A loving and joyful marriage is one in which both partners are intimate with each other. Intimacy is crucial for strong family and marital relationships.
Intimacy means a warm, close, confidential or private relationship, which develops through long association, friendship and familiarity. When we talk about intimacy in marriage, it is that warm, close, confidential or private relationship between husband and wife.
When we talk about intimacy, a woman or man should be the most intimate person with his or her husband or wife. They should be the best of friends. Neither of them should be as close to anyone else as they are to each other. Intimacy indicates the deepest level of privacy that one can think of. Intimacy is what makes marriage to be successful and enjoyable.
Without intimacy, marriage becomes horrible, cold and lonely. Intimacy in a marriage needs to be promoted, to make marriage last a lifetime and remain enjoyable.
God has commanded it for the husband to cleave to or cherish his wife. He will spend time with her to ‘know’ her more. For intimacy to be developed in marriage, both husband and wife should depart from all forms of interferences and cleave to one another, to become one flesh. God’s Word says: For this cause shall a man leave his father and mother, and shall be joined unto his wife, and they two shall be one flesh. This is a great mystery: but I speak concerning Christ and the church (Ephesians 5:31-32). Therefore, you must “leave” so that you can “cleave.” When you do, you are sure to enjoy intimacy in your marriage.
HOW TO ENHANCE INTIMACY
- You Must be OpenTo be intimate with your spouse, there must be no hide and seek game. You must be ready to open up to your spouse, so that your spouse can trust you.
- Embrace TrustTrust is an essential ingredient in our daily living. The very essence of life depends on trust. A marriage cannot survive without trust. Trust is not a gift; it is a virtue that must be built through experience and over a period of time. Trust is reciprocal. The more you express your trust to your spouse, the more he/she responds to you in trust. You must endeavour to believe your spouse.
- Be faithfulTo enhance intimacy in your marriage, you must be faithful to your spouse. Learn to keep secrets concerning everything your spouse tells you (Proverbs 28:20).
- Express LoveBe willing to express your love to your spouse, more than anyone else. Let your spouse be your close confidant. Communicate and discuss issues with your spouse.
- Be Good Listener & CommunicatorYou must be a good listener. When your spouse is talking, you must not be too busy to listen to him or her. Be ready to listen, discuss and make some contributions as well. Engage in an open communication. Open communication is the ability to discuss anything with your spouse. It includes sincere expression of thoughts, feelings, as well as careful listening.
- Be AvailableYou must be willing to make yourself available to your spouse, whenever he/she needs you. No matter how choked up you are in activities, you must create room for him/her, by making yourself available. Learn to spend quality time with him/her. For fun, go out or stroll out together, play games together, etc (Songs Of Solomon 2:4).
- You Must be CaringYou must be ready to express a genuine concern for your spouse’s well-being. If you do things you know hurt your spouse, you cannot have a healthy intimacy. You can develop a more caring heart and mind, by learning to think of your spouse’s feelings before yours. Always ask yourself before acting or speaking, “If I do this or say this, will I hurt my spouse?”
BENEFITS OF INTIMACY
- It brings about unity, which promotes God’s presence and blessings in a marriage Psalm 133:1says: Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity!
- It brings about free flow of communication (Proverbs 27:19).
- It promotes longevity in a marriage (Proverbs 31:11, 28-31).
- It makes marriage more enjoyable (Proverbs 31:5; Isaiah 62:5).
- It brings about greater spiritual strength (Ecclesiastes 4:9-12).
The grace to build a strong intimacy with your spouse is available, when you are saved. You get saved by confessing your sins and accepting Jesus as your Saviour and Lord. If you are ready to be saved (born again), please say this prayer:
Dear Lord, I come to You today. I am a sinner. Forgive me of my sins. Cleanse me with Your precious Blood. I accept You as my Lord and Saviour. Thank You for saving me. Now I know I am born again!
Congratulations! You are now born again! Till I come your way next time, please call or write, and share your testimonies with me through:
- Congratulations! You are now born again! Till I come your way next time, please call or write, and share your testimonies with me through:
- E-mail: faithdavid@yahoo.com
- Tel. No: 234-1-7747546-8; 07026385437; 07094254102
Friday, January 24, 2014
USHUHUDA WA NYISAKI
USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU NA NYISAKI CHAULA
S.L.P. 2262
UYOLE – MBEYA
TANZANIA
YALIYOMO:
UTANGULIZI:
Sura ya 1: Kuitwa
Sura ya 2: Jehanamu sehemu ya kwanza na Mangojeo ya Wafu.
Sura ya 3: Jerusalem Mpya.
Sura ya 4: Mangojeo ya Jehanamu sehemu ya Pili
Unachotakiwa kufanya.
UTANGULIZI:
Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si wa madhehebu yao wala hawajulikani makanisani. Sasa ninakuomba ewe msomaji, tafuta mahali pa utulivu, mwombe Mungu na kusoma ushuhuda huu ili upokee kile ambacho Bwana amekuletea leo.
Msichana Nyisaki Chaula alionyeshwa na Bwana ushuhuda huu akiwa na umri wa miaka 16 mara baada ya kuhitimu elimu ya msingi. Ushuhuda huu alionyeshwa akiwa ameokoka na si kwamba alikufa bali aliona maono. Maono haya alionyeshwa kati ya tarehe 30 – 31/12/1991; yaani kwa siku mbili tofauti.
Msichana huyu hivi sasa ameolewa na Mwinjilistii Lemsy Mheni pale Uyole Mbeya kwa lengo la kukuza huduma yao. Kabila lake ni Mkinga wa Makete, Msichana huyu anapatikana Uyole njia panda ya Malawi – Zambia na Dar es Salaam pembeni mwa kituo cha mafuta ya magari pale Uyole, Bwana awatangulie katika usomaji.
SURA YA 1
KUITWA:
Ilikuwa ni mwezi wa 12/1991 tulipochaguliwa vijana 10 kuombea Mkutano wa Kiroho ambao ulikuwa ukifanyika pale Uyole. Siku moja baada ya maombi ya usiku, nilala pamoja na dada zangu. Siku hiyo nilala usingizi mzito ambao sijapata kuona. Usiku nilishangaa kukuta usingizi umetoweka kabisa, hivyo nikabaki nikiwa macho, ndipo nikasikia sauti ikiita ‘Nyisaki’ nikasikia lakini sikuitikia, ikaita mara ya pili pia sikuitika. Hata mara ya tatu ndipo nikaitika kisha nikasikia ile sauti ikisema ‘Nimekuchagua kuwa mtumishi wangu’ ndipo nikatambua kuwa ni sauti ya Bwana, nikasema â€Å“Bwana mimi ni motto mdogo tena hata chuo chochote sijaenda nitawezaje kuifanya kazi hiyo? Bwana akaniambia mkumbuke Yeremia mtumishi wangu nilimchagua angali bado mdogo (Yeremia 1:5) basi nikaendelea kubishana na ile sauti hadi dada yangu mmoja aliamba na kusema ‘Mshukuru Mungu kwa sababu amekuchagua wewe’.
Ndugu msomaji kumbuka kuwa sauti hiyo nilisikia nikiwa macho kabisa na wala haikuwa ndoto na baada ya kusikia sauti hiyo mara ya pili na ya kwanza niliamka na kuthibitisha kabisa kuwa wote niliokuwa nimelala nao bado wamelala. Na hata huyo dada yangu alisema ‘Mshukuru Mungu kwa sababu amekuchagua wewe’ nilitambua kuwa ni Mungu ndiye aliyemuelimisha na kumfunulia jambo hili.
Baada ya yote haya tukamshukuru Mungu na kulala. Kesho yake tarehe 30/12/1991 ndipo nilipoonyeshwa mambo makuu ya ajabu (Yeremia 33:3)
SURA YA 2
JEHANAMU SEHEMU YA KWANZA NA MANGOJEO YA WAFU:
Ikiwa tarehe 30/12/1191 tulipoamka tukaenda kwenye semina na baada ya ile semina tuliamua kwenda kumuona rafiki yetu aliyeokoka ambaye kwa muda ule alikuwa hajiwezi yaani alikuwa anaumwa. Tulipofika pale nyumbani tukafungua ibada kwa maombi kisha tukaanza kujifunza jinsi Biblia inavyosema kwa njia ya maswali. Hata baada ya hapo tukaamua kufunga Ibada kwa maombi kama tukivyofungua.
‘Tufunge kwa maombi na kumkabidhi ndugu yetu mikononi mwa Bwana, maana tulianza ibada yetu kwa kumshukuru Mungu kwa kuwa ndugu yetu alikuwa hajambo’ Ninachokumbuka ni kwamba tuliimba pambio moja ya kuabudu lakini sikumbuki kwamba tuliingia kwenye maombi au la tulipokuwa tunaimba ile pambio ya kuabudu, nikashangaa kuona kuwa nimechukuliwa niko sehemu tofauti kabisa na mazingira ya nyumbani.
Ukiniuliza kuwa nilichukuliwa vipi hata mimi mwenyewe sielewi, lakini nilishangaa kuona kwamba niko kwenye bonde moja kubwa sana, na lile bonde lilikuwa halina miti wala majani wala ndege na vitu vilivyopo duniani, sehemu yenyewe ilikuwa haivutii hata kidogo, ni sehemu moja iliyokuwa na ukimya wa aina yake. Sasa nikashangaa mbona nilikuwa na rafiki zangu na sasa siwaoni, nikaendelea kujiuliza ni nani aliyenileta huku, na hapa ni wapi? Basi niliamua moyoni mwangu kuwa liwalo na liwe kwa sababu sijui hata aliyenileta mahali hapa, nilikuwa nimekata tamaa, nikajiandaa kutaka kukaa ndipo nikasikia sauti nyumba yangu ikisema ‘Nyisaki nifuate’. Nilipoinuka nilishangaa sana kumuona mtu mmoja mfano wa mwanadamu nilipomtazama yule mtu, umbo lake hakuwa mrefu sana wala hakuwa mnene sana, alikuwa ni mtu ambaye sijawahi kumuona popote duniani. Nywele zake zilikuwa ndefu na alikuwa amezibana nyuma kwa banio jekundu, alikuwa amevaa vazi refu mpaka miguuni na jeupe sana ambalo hata weupe wake sijawahi kuuona hapa duniani. Alikuwa ni mweupe sana, siyo weupe wa hapa duniani, macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, huyo mtu alikuwa hakanyagi chini bali alikuwa akitembea hewani na vazi lile lilikuwa liking’aa sana haliwezi kabisa kutazamika kwa macho ya binadamu. Nayasema mambo ambayo niliagizwa niyaseme, huyu mtu alikuwa amejifunga mkanda mmoja mwekundu kiunoni ndipo nikaamka nikaanza kumtuata. Baada ya hatua chache nikaanza kusikia muungurumo Fulani ambao ulinitisha kwa kiasi Fulani lakini sikuuliza. Kadiri tulivyozidi kutembea mbele ndivyo muungurumo ulivyozidi kuongezeka na kutisha zaidi, mara nikasikia sauti yangu ikiniambia inua macho na tazama mbele, ndipo nikashituka sana nilipoona moshi mkubwa mnene na mweusi umefunika bonde lile na kusababisha giza nene katika bonde. Nikamuuliza yule mtu huko mbele kuna nini? Yule mtu akasema, ‘hiyo ni Sehemu ya Jehanamu watakakoenda watenda dhambi baada ya maisha ya duniani’ Baada ya kusikia hayo yote ndiyo nguvu zikaniishia, nikaanza kulia na kumuomba sana Mungu anisamehe maana kwa mawazo yangu nilifikiri nimekufa na sasa napelekwa Jehanamu nikaendelea kulia sana hadi yule mtu aliponieleza usilie maana ukilia utashindwa kuwafikishia watu wangu habari hizi. Hofu ilijia nilitishika mno, lakini mpango wa Mungu kunionyesha mambo haya ni kuwaambia watu.
Ndugu msomaji, kweli Jehanamu ninavyoelezwa kuwa ni ziwa la moto elewa hivyo. Nilipotazama sikuona mwisho wake, bali niliona milipuko mikubwa sana na ya kutisha na milipuko hiyo haikufanana na milipuko yoyote hapo duniani labda kwa sehemu inayoweza kulinganishwa na milipuko ya visima vya mafuta.
Milipuko hiyo ni mikubwa na inatisha mno iliyosababisha moshi mkubwa sana ulioambatana na moto wa kupaa juu. Moto ule ulijichanganya changanya kama vile bahari iliyochafuka. Kulikuwa na mawimbi makubwa na ya kutisha na yakichanganyika na kutoa miungurumo mikubwa ambayo haiwezi kumfanya mwanadamu kusikia hata mateso ya mwenzake. Mimi nilipokuwa nasikia habari ya Jehanamu nilifikiri labda ni moto mdogo au makaa ya moto. Lakini siku hiyo niliyoona mwenyewe kiasi kwamba nilibaki kulia na kuomboleza kwa uchungu mkubwa mno. Mtu yule alifanya kazi ya kunionya nisillie, pia alinitia nguvu na ndipo nilipoweza kuendelea, ndugu yangu ukisikia Jehanamu iogope kama ulivyo.
Nilipoangalia ndani ya ule moto niliona vitu vyenye uhai virefu vyeupe nikauliza hivyo ni vitu gani? Yule mtu akasema ‘hao ni funza wa Jehanamu’ hizo rangi kwenye pingili zake ni za nini? Akasema hivyo siyo rangi, kama unavyowaona hao funza wana meno hayo manne yenye uwezo hata wa kutoboa fuvu la kichwa cha mtu, na huyo funza akishaingia ndani huacha sumu kali (yahani hiyo unayoiona kama rangi ambayo humtesa mwanadamu milele na milele.
Hao funza walikuwa ni wengi sana lakini hawafi ndani ya ule moto, (Marko 9:45-46) walikuwa wembamba warefu yapata mita moja, na walikuwa na pingiri pingiri ambazo zilionekana kuwa na rangi, walikuwa na meno mawili mbele na kichwani kulikuwa na meno mawili jumla ya meno yote manne, yaani mkiani na kichwani kulikuwa na midomo.
Bwana akasema ‘ hawafi wala hawaugui kwa sababu wamehifadhiwa kwa ajili ya mateso ya watenda maovu’
Ndugu msomaji, nisingeweza kupoteza muda wangu kukuletea jambo ambalo sijaliona lakini nimesema haya ili ukiwa na masikio na uyasikie, ukikataa ni juu yako mwenyewe. Maana sikuambiwa kwamba nimlazimishe mtu aokoke, bali niliambiwa nikamwambie kila mtu labda atakuwepo mmoja atakayegeuka na kuponywa. Sasa nikauliza mbona watu wanasema Jehanamu kuna wanaoungua lakini iweje Jehanamu hii haina watu wanaungua? Akasema wanasema kweli lakini watu watakuja kutupwa kwa wakati wake. Lakini muda huu wamehifadhiwa wakimsubiri baba yao aliyewadanganya (yaani shetani).
Akasema twende nikakuonyeshe nikaanza kumfuata. Kweli ndugu zangu Jehanamu uisikie kama ilivyo. Nilipofikiri habari za wale funza wa ajabu kwa kweli nililia kwa uchungu mkubwa mno nilitetemeka na kuishiwa nguvu nikaanza kuwaza moyoni mwangu mtu anayejua dhambi ni mbaya, na anajua neema ya Mungu na kupuuzia kweli uje kuteswa katika ziwa hili la kutisha lenye moto usiozimika na funza ambao hawafi, kwa kweli nililia sana. Lakini yule mtu akaniambai nyamaza, maana ukilia utashindwa kuyafikisha yote ninayotaka kukuonyesha. Kwa kweli nashindwa hata nieleze vipi. Jehanamu ni kweli ipo na inatisha sana; achana na mafundisho ya mashetani yanayosema hakuna Jehanamu na ukiendelea kufuata hayo utaangamia na kujuta milele. Ninaeleza ndugu yangu kuwa Mungu hapendi upotee ndiyo maana amekupa nafasi kama hii. Nayo yawezekana ni nafasi ya mwisho sasa usipokubali kutubu yawezekana ukajiletea maangamizi wewe mwenyewe.
JEHANAMU IMEANDALIWA KWA AJILI YA SHETANI NA MALAIKA ZAKE:
Niliondoka sehemu hii ya Jehanamu na kuelekea sehemu ya mangojeo nikiwa nalia kwa uchungu mkubwa mno. Na haya ninayokuambia sikutishi bali nakuambia kweli na kama unafikiri nakutisha basi utakwenda kuona mwenyewe.
Nikaenda kumfuata yule mtu, tulipofika mahali fulani na kutazama bondeni niliona bonde kubwa lililokuwa limefunikwa giza la kutisha mno. Kabla ya kuwafikia wale
watu nilisikia sauti za watu zikilia kwa uchungu mkubwa mno, ndugu yangu kweli Jehanamu kuna vilio vya aina yake, vilio ambavyo huwezi kulia kama walivyokuwa wakilia wale watu, wanalia bila kupumzika. Lile giza nene mno linawafanya wale watu wasiwaze kutazamana kila mmoja na kilio chake na kila mtu na mateso yake hakuna mtu ayakayeondoka kwenda kumfariji rafiki yake, kwa sababu kila mmoja aliomboleza kwa ajili ya mateso yake, kadiri tulivyozidi kuteremka lile bonde ndivyo lile giza lilivyozidi kutoweka.
Ndipo tulipofika kule bondeni niliona watu wengi mno wasio na idadi; ni wengi kama weusi wa duniani, hakuna mzungu wala mwafrika wote ni weusi kupita kawaida. Na weusi uliosababishwa na baridi kali sana inayopatikana sehemu ile. Na ndimi zao zilikuwa zimevutwa hadi kufikia kila mtu kifuani pake, awe mrefu au mfupi. Nikauliza mbona ndimi zao watu hawa zinafika kifuani? Yule mtu akasema unavyoona sehemu hii haina maji wala haina furaha yoyote, sasa hizo ndimi wanazitumia kwa kulamba machozi, machozi haya hupatikana kwa kilio cha miezi mingi sana kupita na ndipo inatokea chozi moja ambalo hulitumia kama maji. Ndipo nikashikwa na uchungu wa ajabu nikakumbuka hawa ni watu walioishi chini ya Neema ya Mungu, lakini baada ya kufa kwao wako sehemu ya Jehanamu wakimsubiri baba yao aliyewadanganya. Kulikuwa na wanawake na wanaume.
Watu wale walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa mno. Nikamwomba yule mtu, nikisema Bwana naomba wachukue watu 100 kutoka kila nchi ili waone hii Jehanamu wawaambie wanadamu watageuka. Akasema wanadamu ni wenye mioyo migumu hata angerudi Yesu mwenyewe wasingemwamini wangeendelea na dhambi. Basi nikaendelea kulia sana. Kisha akaniuliza kama nilikuwa nawafahamu wale watu, nikasema siwafahamu. Akasema twende huku, nikaendelea kukatiza katikati ya mabilioni ya watu waliofia dhambi, kila mmoja na uchungu wake na kila mmoja na mateso yake.
Hata wa kwanza kumuona alikuwa Babu yangu mzaa Mama, yeye alikuwa ni Mwinjilisti na Mzee wa Kanisa katika kanisa la Lutherani kule Isapulamo Makete, sasa nilishangaa sana kumuona katika sehemu hii ya Jehanamu, yeye akiwa duniani alikuwa mweupe sana. Lakini sasa nilishangaa kumuona akiwa mweusi kupita kawaida. Nikamuuliza mbona mtu huyu alikuwa mtumishi wa Mungu na sasa namuona sehemu hii? Yule mtu akasema kweli kabisa huyu mtu alichaguliwa kwa ajili ya kazi ya Mungu lakini aliamua kuifanya kazi ya Mungu na kuingiza michanganyo. Na ndiyo maana ukamuona sehemu hii, ulevi kidogo alikuwa nao, ushurikina kidogo na mambo mengine kama hayo, kama maandiko yasemavyo Ufalme wa Mungu wanauteka wenye nguvu tu. (Matayo 11:12)
Mtu wa pili alikuwa jirani yetu, alikuwa ni kaka mmoja aliyekuwa anasali kanisa la Moraviani. Alikuwa ni kaka mmoja aliyejipenda sana na kila siku ya ibada na Jumapili alishika Biblia na kitabu cha nyimbo, kumbe alikuwa hafanyi mapenzi ya Mungu. Hata leo ukienda Uyole utasikia sifa zake. Huyu kaka alikuwa anaumwa sana na amelazwa katika hospital ya Mbeya, siku mbili kabla ya kufa kwake alituma watu kwenda kumuita mchungaji amwombee na baada ya siku mbili akafa. Sasa nikashangaa sana kumuona sehemu hii ya mateso, wakati huo huo wanasema mtu akiombewa anakwenda moja kwa moja mbinguni? Yule mtu akaniambia kawaambie watu wote duniani, mtu yeyote aliyejua kuwa dhambi ni mbaya na atakwenda Jehanamu, akisema nitatubu, nitatubu nikiona kwamba nimekaribia kufa, mimi huyo simpokei. Jinsi ninyi msivyopokea vitu vilivyooza ndivyo na mimi sivipokei japokuwa navitoa duniani (Ufunuo 22) Yule kaka akasema ninakuomba kawambie mama, baba na ndugu wasitende dhambi japokuwa mimi nimepata bahati mbaya kuja sehemu hii lakini kawaambie wasitende dhambi. Yule mtu aliyekuwa ananiongoza akasema usiende kuwaambia kwasababu duniani kuna wachungaji na waliookoka wanahubiri Injili wasipowasikia hao, nyumba nzima watakuja huku (Luka 16). Yule kaka akajitupa chini akalia kwa uchungu mkubwa mno.
Mtu wa tatu kunionyesha alikuwa Mama yangu mdogo upande wa Mume wangu (Alipokuwa anasafiri mme wake) akakorofishana na wakwe zake ( yaani wazazi wa mume wake) basi akanywa vidonge akafa, mume wake aliporudi na kuonyeswa kaburi mkewe akachukua vidonge akanywa sasa tulipokuwa tunaenda kwa rafiki yetu kumuona ndipo tulipishana na gari iliyokuwa inampeleka hospitali akiwa mahututi. Sasa nikashangaa sana kumuona katika ile sehemu ya mangojeo. Nikauliza huyu mtu niliyemwacha duniani na sasa namuona huku? Yule mtu akasema, kawaambie ndugu zake duniani, mtu anapokufa duniani ile sekunde moja tu, huku amekuwa ameshiriki kiasi cha kutosha, kama ni mtu wa uzima amekuwa na uzima na amekuwa mwenyeji, sasa huyu mtu hapa unavyomwona hata dakika kumi na tano hajamaliza. Nilishangaa sana maana alikuwa mweusi sana, ulimi wake umevutwa na kufika kifuani kama wale wengine. Alionekana kama mtu aliyekaa kwenye mateso yale zaidi ya miaka elfu kumi. Moyo wangu ulijaa huzuni na uchungu usio wa kawaida, basi yule mtu akaniambia sasa ‘kawaambie watu wote jinsi ulivyoona, na jinsi ulivyosikia usiongeze wala usipinguze atakayekataa usimlazimishe wala kumbembeleza, atakayekubari mwongoze sala ya Toba’.
Ndipo nikashangaa natokea katika nyumba ya yule rafiki yetu, wenzangu wote wametulia wakisubiri litakalotokea basi nikawaeleza yote niliyoyaona na kusikia basi tukamshukuru Mungu.
SURA YA 3
YERUSALEMU MPYA:
Siku ya tarehe 31/12/1991 niliongozwa na Mama kwenda shambani. Nilimweleza habari zote za baba yake, lakini mama hakuwa na la kufanya zaidi ya kusikitika, kwa maana nafasi ya baba yake ina gharama wala haina budi kuiacha hata milele (Zaburi 49:7-8)
Baada kufika shambani nilichimba shimo la kwanza, la pili na tatu kwa ajili ya kupanda mahindi, mara nikaanza kujisikia vibaya, basi nikamwambia mama akasema mwanangu hivi sasa ni saa tatu asubuhi watu wakikuona unarudi nyumbani watashangaa sana, vumilia kidogo. Sasa sikumbuki kama niliongeza kuchimba shimo au hapana. Nilishangaa niko kwenye sehemu nyingine ya tofauti kabisa na mazingira ya dunia, sehemu hii ilikuwa inaleta matumaini sana.
Sehemu hii ilinivutia mno basi nikawaza moyoni kama asipotokea yule mtu wa jana nitang’ang’ania huku huku. Nikaamua kukaa mara nikasikia sauti nyuma yangu ikisema ‘tufuate’ nilipogeuka nikashangaa kuwaona watu wawili waliofanana sana na mtu wa jana katika hali zote. Mmoja ameshika upanga na alisema anaitwa Mikaeli na aliyekuwa ameshika karatasi alisema alisema anaitwa Gabriel, Wasomaji wa Biblia wanajua kazi zao (Daniel 10:13, Yuda 1:9, Luka 1:26)
Nasikia sauti ndani yangu ikiniambia, inua macho yako utazame mbele nilishangaa sana kuona mbele yetu kulikuwa na nuru kubwa sana kutoka katika mji mmoja mkubwa na mzuri ajabu. Nuru ile iliangaza vizuri kuliko hata mwangaza wa jua na mwezi. Kwa kweli nilivutiwa sana na mji ule jinsi ulivyo na unapendeza. Nikauliza ule mji ni mji gani? Na ni kwa ajili ya nini? Wakaniambia ‘Ule ni mji Mtakatifu, Yerusalem mpya na ni kwa ajili ya Watakatifu walioshinda ya dunia’ Kwa kweli nashindwa hata kuelezea uzuri wa mji ule maana hauna mfano wa aina yoyote hapa duniani. Tumani langu ni kwenda kuishi katika mji wa utukufu mwingi sijui mwenzangu unatumaini gani?
Tulipofika mlango wa lile jiji, mawazo yangu yalinipeleka moja kwa moja katika tenzi namba 121 ‘’Liko lango moja wazi’’ Niliona lango moja kubwa lililokuwa wazi, (Ufunuo 3:7-8) lango hili lilikuwa likibadirika kila aina ya rangi, nyingine hazipo duniani. Tulipoingia ndani karibu na mlango tulimwona mtu mmoja mzuri sana mweupe na aling’aa sana, alikuwa amekalia kiti kizuri na cha thamani kupita kawaida. Alionekana kuwa mtu mpole mwenye huruma sana na upendo, (Mithali 11:28-30) tabasamu lake lilinipa raha ya aina yake na kuifanya nicheke sana kwa furaha na kujisahau. Malaika nilioongozana nao walianza kuzungumza na yule mtu kwa lugha nisiyoifahamu. Mimi nikaendelea kushangilia ule mji, ule mji umetengenezwa kwa vioo vitupu. Kila sehemu nilipotazama nilijiona mwenyewe (Ufunuo 21:18) nikaendelea kushangilia ule mji kwa uzuri wake na thamani yake hadi pale wale malaika waliponiambia tufuate.
Malaika walinitembeza mji mzima kwa muda mfupi sana hata sekunde moja haikuisha, nilishangaa sana sujui wametembea vipi wale watu. Malaika wa Kwanza akafungua mlango akaingia wa kwanza, pili nikaingia. Katika sehemu hii niliviona viti vingi sana vilivyokuwa vimeandikwa majina kwa damu mbichi. Vile viti vilikuwa vizuri na vya thamani kupita kawaida. Nikaomba kukalia kiti kimoja nikaambiwa utakalia ukishinda ya duniani.
Katika sehemu zote sikuona taa zikiangaza lakini kulikuwa na mwanga mzuri sana. Nikauliza mwanga huu unatokana na nini? Akaniambia mwanga huu ni wa mwanakondoo uliyemkuta mlangoni.
Nilipoingia kila mahali niliduwaa kwa kustaajabu ule uzuri wa mji ule. Kila mlango ulibadili baina ya rangi. Tukaondoka sehemu hii. Akafungua mlango mwingine nikastaajabu kuona bustani nzuri sana iliyozungukwa na maua ya majani yote yalikuwa na urefu sawa bila kuzidiana. Tena yalikuwa ya kijani kibichi sana. Maua ya sehemu hii marefu na yanamsifu Mungu kupita kawaida, yakiinama upande wa kulia yanakwenda yote na kusujudu na kuinuka hutoa harufu nzuri sana inayoenea mji mzima, maua hayo yalikuwa yamezungukwana kioo. Nikasema naomba nichume ua moja nikawaonyeshe ndugu zangu. Akasema maua ya huku hayachumwi, nikasema bustani hii imetengenezwa kwa hajili ya utukufu wa Mungu, nilitamani sana kukaa sehemu hii ya bustani, lakini wakasema tufuate.
Kila mahali tulipokwenda mmoja akafuata mwingine, nikasikia sauti nzuri mno zikiimba kwa furaha sana tukaingia, nikashangaa sana kuona watu wengi sana wasio na idadi. Nikajiuliza kwa nini Mungu anasumbuka kuwatafuta wanadamu wakati anao wengi sana? Nikastaajabu sana nikakumbuka pambio moja inayosema; Ukiringaringa kwa Yesu kuna watu wengi. Hawa watu walikuwa wanadamu kama sisi ambao waliishi duniani, lakini wao walimwishia Mungu na kufa na utakatifu.
Kama umewahi kuona mapacha basi wale ni mapacha wa aina yake. Sura zao hazitofautiani hata kidogo wamefanana sana hisivyo kawaida. Nywele zao zilikuwa ndefu wamezibana na banio jekundu sana, wala si wembamba sana na milifanikiwa kugundua tofauti moja tu. Wengine wamevaa mikanda miwili kiunoni na wengine mkanda mmoja. Nikauliza kuna tofauti gani kati ya waliovaa mkanda mmoja na waliovaa mikanda miwili? Akasema waliovaa mmoja ni wanaume na waliovaa miwili ni wanawake. Lakini ilikuwa sio rahisi kuwatofautisha kuwa huyu ametoka Taifa hili na yule Taifa lingine, waliimba wimbo mzuri isivyo kawaida, staili za uimbaji wao kwa kweli zilinifurahisha mno, walipunga mikono yao wote kwa pamoja na hapakuwepo hata mmoja wao aliyekosea. Nilipozidi kuwatazama nilitamani sana kujiunga nao ili nami niimbe na kumsifu kama wao wanavyosifu, lakini haikuwezekana kwa sababu hata lugha yao nilikuwa siijui. Baada ya muda akatokea dada mmoja na kuja upande wangu, niliweza kujua ni mwanamke kwa sababu alikuwa na mikanda miwili, nilishangaa kumuona yule dada kwa sababu niliweza kumtambua baada ya sura yake ile ya duniani kutokea. Yeye alikufa mwaka 1987 mwezi wa nne na aliuawa kwa kupigwa risasi. Yeye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari (Mbeya Day) kidato cha tatu (Form Three). Aliponifikia alisema ‘Ah Nyisaki, umekuha huku’ nikasema ‘Ndiyo’ akasema ‘Za duniani’ nikasema ‘Duniani matatizo’, akasema ‘Kweli matatizo. Angalia wenzenu tumevikwa miili mipya isiyoharibika, isiyopata magonjwa’ yaani aliusifu mwili wake na ni kweli ndivyo alivyo (1Korintho 15:40-53) akasema ‘Mwili wa zamani tumeuacha pale’, basi nikageuka niangalie amesema wapi, kweli ndugu yangu Biblia inasema mtafuteni Bwana maadamu anapatikana, mwiteni maadamu ya karibu (Isaya 55:6-7) mambo ya Uyole niliyaona kama vile unavyoweza kutazama kitu kwenye kiganja chako. Nilipoangalia sokoni nikaona biashara zinaendelea kama kawaida, barabarani magari na baiskeli ziliendelea kupishana kama kawaida, nilipotazama makaburini aliponionyesha huyu dada, nikaona makaburi ya watu wengi tena niliweza hata kusoma majina yao. Pia niliweza kujua wazi kabisa kuwa huyu yupo uzimani au jehanamu. Na kama hayupo ilionyesha wazi yuko uzimani. Kaburi la huyu dada lilionekana pia likiwa limepambwa maua. Akasema ‘umekiona kile kitu?’ Nikasema ndiyo, akasema ‘Ule ni mwili wako’. Kwa kweli sikupenda kuutazama mwili mara mbili, mwili wangu niliuona kama ngozi ya kenge chafu sana akaniambia geuka tena, nikakataa, mara ya pili nikakataa, mara ya tatu nikageuka nikaona kama mtu analima na kupanda mbegu akasema yule ni mama yako, fahamu zake tunazo huku, atarudishiwa fahamu utakaporudi wewe. Maono ya siku hiyo yalikuwa ya muda mrefu, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Nilipochukuliwa kwenye maono mama alibeba mwili wangu kuweka kivulini, hapo ndipo nilitambua kweli fahamu zake zilichuliwa. Yule dada akasema Nyisaki kawaambie ndugu zangu wasitende dhambi tena katika mji huu hakuna huzuni, lakini ninawaona wanaendelea na dhambi nasikitika sana, wale Malaika wakasema ‘Usiende kuwaambia kule kuna walio’koka wanahubiri Injili, wasipowasikia hao basi ’
Mtu wa pili kunionyesha alikuwa mzee mmoja wa makamo aliyedharauliwa sana pale Uyole, alidharauliwa kwa sababu yeye alikuwa rafiki wa Biblia na Tenzi za Rohoni na kila alipojipumzisha iwe ni shambani, nyumbani au sehemu nyingine yoyote alisoma Biblia, aliimba Tenzi na kuomba, kweli yule alijishusha (Luka 14:35, 18:17, Isaya 51:7-8) watu walisema amechanganyikiwa. Nilishangaa kumuona katika sehemu hii akiwa kama kijana wa miaka ishirini (20), naye pia aliusifu mwili wake isivyo kawaida, kweli miili ile ni mizuri sana akasema kawaambie wapendwa wa duniani kila mmoja ajitahidi ashinde ya duniani maana muda umeisha, (Ufunuo 22:10-14) kila mmoja aangalie shetani asimpumbaze maana tuna hamu kubwa kuwaona wapendwa wetu, akaondoka akachanganyikana na wenzake.
Akatokea mtu wa tatu naye nilimtambua kuwa ni mwanaume kwa sababu ya ule mkanda mmoja, aliponikaribia ikatokea sura ya duniani, yeye alikuwa mzee wa Kipentekoste, alikuwa anasali Kanisa la Assemblies, akasema ‘Ah Chaula umekuja huku’ nikasema ‘Ndiyo’, ‘Za duniani?’ ‘Duniani matatizo’ akasema ‘Kweli matatizo, angalieni wenzenu tumevikwa miili mipya isiyosikia njaa, isiyopata magonjwa’ Basi aliusifu ule mwili, kweli alikuwa amebadirika naye alionekana kama kijana wa miaka ishirini (20) baada ya hapo akaondoka akaendelea kuimba. Baada ya kuonana na hao watu nikawauliza hao Malaika, hivi hawa watu wanajifunza kuimba? Wakasema kwa nini unasema hivyo, nikasema wanaimba wimbo hauishi akasema sivyo kama mnavyoimba duniani, maana duniani mkiimba dakika tano mnasema tumemsifu sana Mungu na wengine wanadhani wataenda mbinguni kwa sababu ya uimbaji bila kuokoka. Wimbo mmoja wa huku unaimbwa kwa miezi tisa, beti moja miezi mitatu, ‘’Chorus’’ miezi mitatu na beti ya mwisho miezi mitatu, basi nikashangaa sana. Tukaondoka hii sehemu akasema twende nikakuonyeshe watakatifu waliokuwako mwanzo wa kanisa, maana wameletwa sehemu yao akafungua mlango, tukaingia nikaonyeshwa watu kumi na sita (16), lakini nilijua wazi walikuwako na wengine zaidi
Mtu wa kwanza alikuwa Batholomayo, naye akanikumbatia na kunishika mkono, akasema Bwana ndiye aliyechunwa ngozi kwa sababu ya Injili. Na mtu wa pili kunionyesha alikuwa ni Yohana Mbatizaji, nikasema ndiye aliyekatwa kichwa kwa sababu ya Injili, akasema ndiye huyu. Basi akanikumbatia na kunishika mkono (Mathayo 14:1-11). Mtu wa tatu kunionyesha alikuwa ni Eliya Mtaabishaji wa Israel (1Wafalme 18:17-18) naye akanikumbatia na kunishika mkono, alinionyesha wengi sana akina Paulo, Petro na Yohana na wengineo. Batholomayo akasema, ‘Mpendwa, kawaambie wapendwa duniani, wakaze mwendo maana sekunde moja siyo muda mrefu’ (Filipi 3:12, 1Korintho 9:24-27), tukaondoka ile sehemu.
Wakanipeleka sehemu ambayo zinaandaliwa nguo za kuvaa watakatifu katika karamu ya Mwanakondoo, katika sehemu ile niliwakuta malaika wengi mno wakimsifi Mungu kwa shangwe. Katika sehemu hii pia kulikuwa na mashine nzuri zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu mno, nguo nyingi sana ziliingia ndani ya mashine na kutolewa zikiwa zinang’aa sana, nikauliza mbona nguo zinatengenezwa nyingi sana, ni za nani? Maana watu wengi wanakataa wokovu. Akasema ‘Ninyi kaihubiri injili tu, anayetaka kuokoka na aokoke asiyetaka aache, kinachotakiwa ni kwamba anapokuja Mwana wa Adamu asiwepo wa kusema mimi sikusikia’
Basi tukaondoka ile sehemu. Ule mji ni sifa kila kinachofanyika, kilifanyika huku wakimsifu Mungu, si malaika wala si mwanadamu, si maua, si vinanda, maana vinanda vya kule vinapiga vyenyewe. Wakanipeleka katika ile sehemu ya awali iliyokuwa na viti vingi vyenye majina yaliyoandikwa kwa damu mbichi.
Tulipofika mara ya kwanza hakukuwa na mtu, lakini muda huu tulimkuta mtu mmoja aliyekuwa akifanya kazi kwa haraka sana, alikuwa amekazana sana kuliko Roboti. Nilimwuliza katika mji huu kuna watu wawili kama hawa? Tena kwa nini wamekazana sana hivi. Akasema huyu ni mtu mmoja kumbuka alipokuwa anaondoka duniani alisema, Ninakwenda kuwaandalia mahali ili alipo nanyi muwepo. (Yohana 14:1-6), akasema ‘huu mji ameuandaa mwenyewe hakuna mtu aliyemsaidia. Tena amekazana kwa sababu muda umefika wa kuchukua walio wake duniani’ (1Thesalonike 4:13-17). Wakaniondoa sehemu hii. Sehemu inayofuata ni sehemu muhimu sana, umesoma na kusikia zote za kwanza, sasa naomba utulie.
SURA YA 4
MANGOJEO NA JEHANAMU YA PILI:
Mmoja wa wale malaika akaniambia sasa tunakwenda kukuonyesha Jehanamu sehemu ya pili nikasema, Ah kuna sehemu nyingine tena? Akasema ‘Ndiyo, hii imezishwa ukari mara saba zaidi’ (Mithali 15:10).
Baada ya mazungumzo hayo, ndani yangu furaha ya uzima wa milele ikatoweka nikawaza iwapo sehemu ile nililia vile? Je hii itakuwaje? Nikawafuata katika sehemu hii ya mangojeo peke yake ilinitoa raha, kwa sababu ilikuwa ni kama mara saba zaidi ya ile ya kwanza. Watu wake walitoa sauti za uchungu mkubwa mara saba zaidi, watu niliowaona ni wale wote waliozijua siri za Mungu na kudharau, ni wale wote waliookoka na kuacha wokovu. (Ebrania 2:3, 6:4-6) Ni mchungaji na waalimu (Yakobo 3:1, Ezekieli 34:2-6) wanalia milele na milele bila kutoa chozi moja. Kabla hata ya kuonyeshwa nililia kwa uchungu sana na kuishiwa nguvu.
Akainuka mtu wa kwanza akasema, Bwana naomba umtume mtumishi wako aniletee tone la maji niuburudishe ulimi wangu. Mpendwa habu jiulize wewe upo duniani, je unaridhika na tone moja la maji? Basi sehemu ile tone la maji lina thamani sana wanalilia tone hilo usiku na mchana.
Malaika akawaambia mlipokuwa duniani mliichezea neema ya Mungu, sasa hivi ni sehemu ndogo sana ya mateso bado sehemu yenyewe. Yule mtu akajitupa na kuendelea kulia kwa uchungu mno nilimwangalia tena haikuinuka kabisa.
Nikaendelea kuwafuata wale watu huku nikilia na kutembea kwa taabu mno tukamkuta mtu wa pili akasema, Bwana utupe sekunde 10 tukaihubiri injili ulimwenguni ili waokoke. Yule Malaika akasema mlipokuwa duniani mlikuwa na muda mwingi sana wa kuihubiri injili lakini mliutumia kwa tama zenu sasa hii ni sehemu ndogo tu ya duniani nikalia kwa uchungu sana. Hakuinuka tena, mateso waliyonayo yanawafanya waombe sekunde 10 kuhubiri.
Mpendwa muda uliopoteza kwa mambo yasiyo ya maana utadaiwa, maana wewe ungehubiri injili Jehanamu ingekosa watu wa kwenda kwa sababu umetumia vizuri muda wako kuhubiri injili.
Mara nikasikia kigelegele cha kutisha mno nikauliza hivi, kuna mtu ametupwa motoni? Wakasema hapana. Tumesema jehanamu hii imezidishiwa ukali mara saba zaidi. Sasa kigelegele hicho ni cha moto kikishangilia kwa sababu muda wake umefika. Nikasikia mara nyingine tena, nikauliza vilevile nikaambiwa mbona wewe husikii, jehanamu hii imezidishwa mara saba zaidi. Wale watu wanasikia vigelegele vya kutisha lakini hawana la kufanya zaidi ya kusubiri mateso, tofauti na duniani ambapo mtu akipata shida kidogo anajiua, lakini sehemu hii haiepukiki. Tofauti nyingine tena ni kwamba duniani mtu anayo nafasi ya kutubu, lakini sehemu hii hakuna.
Ndani ya ule moto niliwaona FUNZA waliokonda sana, basi nikasikia sauti kutoka upande ule ikisema Bwana ‘watu uliosema utawaleta watakuja lini?’ Nikashituka na kuuliza je huku kuna mtu, funza hao waliongea lugha ya Kiswahili. Akawaambia wale funza subirini kidogo, hapo ndipo walipoonekana kuwa wamechokozwa. Hakukuwa na maelewano kabisa, walipiga kelele wakisema ‘chakula chetu’.
Akaniambia hao funza ulivyowaona wamekonda watakapomshika mwanadamu ipo kazi. Nililia sana hadi wale malaika wakaamua kuniondoa sehemu ile; akasema ‘sasa kawaambie watu wote duniani, usiongeze wala usipunguze’. Nikasema Bwana mimi duniani siendi wala hapa sikai nipeleke kwa wale wanaoimba. Basi akanigusa bega, nikashangaa natokea shambani saa kumi na mbili jioni na mama ndipo aliposhituka na kuja kuniona.
Sasa ndugu yangu, nimekueleza jinsi ilivyokuwa na sasa ni juu yako wewe kuchagua, sikuongeza wala sikupunguza (Mathayo 7:13-14, Kumbukumbu 3:19-20).
MIMI SITAONGEZA NA SASA NI KAZI KWAKO KUAMUA (Ufunuo 3:20)
MUNGU NA AKUBARIKI.
MAMBO YA KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYA UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA
Jambo la kwanza
Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusiano
wako na wazazi wako.
Mwanzo.2:24 anasema, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja”. Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, “Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie”.
Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako. Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako. Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako.
Na kabla hujafikia maamuzi ya namna hiyo - ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu. Maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi ambacho maamuzi yako yoyote unayofanya lazima ushirikiane nao, na hiyo ni hatua nzuri kabisa. Lakini ukiishaingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza wakushirikiana naye ni mke wako kama umeoa, na ni mume wako kama umeolewa lakini, sio baba yako, sio mama yako.
Na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, wanataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako, haiwezekani. Biblia inakataa. Sasa ukisoma ile Mwanzo unaweza ukafikiri ni wanaume tu wakioa ndio wanatakiwa watoke, waachane na wazazi wao, lakini Zaburi 45:10,11 inatuambia wazi kabisa, inasema, “Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye Mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie”.
Sasa haimaanishi usiwasalimie, haimanishi usiwasaidie, lakini ningekuwa nazungumza kwa kiingereza ningekuambia, “your priorities must change” lazima ubadilike jinsi ambavyo unaweka kipaumbele katika watu ulio nao.
Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako. Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako basi bado hujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu. Maana biblia inasema, kabla hujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.
Sasa kuna tofauti ya kupenda na kutamani. Kabla hujaolewa au kabla hujaoa huruhusiwi kutamani. Lakini ukiisha oa unaruhusiwa kutamani lakini mke wako tu. Ukiishaoa kutamani mke wako ruksa, na biblia imeweka vizuri kabisa, na ukiishaolewa kutamani mume wako ni ruksa. Lakini biblia imeweka utaratibu wa ajabu sana kwamba, ili mume amtamani mke wake, lazima mke wake awasahau kwanza watu wa nyumbani mwa wazazi wake. Hiki ni kigezo kigumu sana.
Ndio maana unaweza ukakuta mtu ana mke mzuri sana lakini hamtamani. Unaweza ukafikiri labda ni kwa kuwa hajajipamba vizuri; lakini hata kama atajipamba, atajikwatua kuanzia asubuhi mpaka jioni, - anaweza hata akatumia muda mwingi kwenye kioo kuliko kwenye maombi akijitengeneza, lakini bado mume wake asimtamani; kwa nini? Kwa sababu ndani yake hajaachia watu wa nyumba ya wazazi wake. Au watu wa nyumba ya baba yake wana nafasi kubwa moyoni kuliko mume wake.
Ni mabadiliko ambayo lazima uyatarajie, watu wengi sana huwa hawafikirii hayo, wanafikiri ni kitu rahisi. Unaweza sasa ukaelewa kwa nini watu wengine ikifika siku ile ya “send off”, yaani ya kum’send’ msichana ‘off’ asikae tena nyumbani kwa baba yake, hiyo siku ni ngumu sana kwa wazazi. Kwa sababu wanajua, wanaagana na msichana wao, mahusiano yao waliokuwa nayo toka mwanzoni, tangu alipozaliwa, alipokuwa tumboni mpaka wakati huo yanabadilishwa, yanajengwa mengine, sasa anakwenda kuwa mke wa mtu, hawawezi tena kuingilia maamuzi juu yake, amefunga agano mahali pengine.
Unakuta siku hiyo wazazi wengine wanalia, unakuta vijana wengine wanalia, wasichana wengine wanalia. Usije ukafikiri ni kitu rahisi. Ndani ya nafsi kuna vitu vinaachana, kati ya wazazi na wale watoto wanaoana.
Mwl. C.Mwakasege
CHANZO: INJILI TANZANIA BLOG
Thursday, January 23, 2014
Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa matamanio ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Internet kunawatenga watu kutoka kwa familia na marafiki zao.
Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali. "Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.
Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio nyaya tupu.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.
Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.
CHANZO: BBC SWAHILI
RENEWING YOUR MARITAL RELATIONSHIP (1)
By Pst. Faith Oyedepo
Dear Reader,
You are welcome to this glorious and exciting moment in God’s presence. As you pay rapt attention to God’s Word concerning your marriage today, Him hands shall rest upon your marriage.
This month, we shall be looking at this all-important subject, Renewing Your Marital Relationship. To renew your marital relationship, one of the things that must be in place is your Expectation.
Every man sets a stage for his miracle. It is your expectation that gets fulfilled. One key factor for the miraculous is expectation. Do you totally and truly believe Him? Don’t you doubt Him somewhere in your heart saying,
“I tried everything….but nothing worked. I never saw anything. I am tired. I don’t think it will work.”
“I tried everything….but nothing worked. I never saw anything. I am tired. I don’t think it will work.”
Don’t’ be offended in God, for the fact that you still have the breath of life. Express your mind to God. Say, “Lord God, I thank You. I know You are forever faithful. Thank You for the gift of life. That I still have a mind to know what I could not get last year, and I am still alive today to approach You, I appreciate You. You have even promised me a glorious and fulfilling year ahead of me. I know You will do it.”
Forget about old things; they are old. God will do a new thing in your family, this year, which will make you live everyday of your life thanking Him. God is set, but you have to be set too. To be set, you must determine to do some things, especially, if a successful home is what you desire this year.
- Husband, can you see a turnaround in the character of your wife?
- Can you see your children obedient and God-fearing?
- Can you see abundance of peace, joy and harmony in your home?
- Wife, what do you see?
- Do you see your husband turning from his sinful habits to pleasing God this year?
- Do you see his business going up, and he begins to provide more for the family?
- Can you see serenity in your home?
As far as you can see, it shall be given to you. It is only what you see that you can possess.
Stop seeing the negative. Stop seeing your business going down, because of economic meltdown. Stop deducing reasons why you think things won’t work out well in your family. Stop celebrating failure. Believe God and let it be counted to you for righteousness. If God has said what He will do, let it be settled in your heart and in your actions, that He will do it. He is not a liar!
Many years ago, I made up my mind to believe God’s Word in Proverbs 4:18. I have never had cause to doubt it. No last year has been better than the current one for me and my family. In fact, my present position as at today, is the least I can ever be. God is ever faithful. Friend, see good and you shall have good. See no lack around you this year, and you shall walk in abundance. God will see to it that His Word does not fall to the ground in your own life. Choose to believe God and you will have no occasion to regret.
See with your eyes of faith. Walk by faith and not by sight. Don’t determine the happenings in your home this year by the environment. See into the plans of God for your life and family life, and assure yourself of the best of times ahead.
Someone once came to me for counselling, and had been having a very tough time in her marriage. As she spoke, I discovered that the root cause of her problems was her wrong idea about marriage. She had expected grief and calamity. So, when the storms rose against her marriage, she began to say, “They told me it will be like this.”
You must first desire a tower, before you can plan to build one. Don’t enter into marriage without an expectation. The Word of God says: For surely there is an end; and your expectation shall not be cut off (Proverbs 23:18). What you expect is what you will get. Like God’s servant, Bishop Oyedepo would always say, “Expectation is the mother of manifestation.”
God has promised to grant your expectations, whether good or bad. So, let your expectations be based on God’s Word, for it is higher than any evil experience or information you may have had or heard about marriage.
If you are already married, there is still an opportunity for you to change all your negative expectations. As a couple, discuss your positive expectations and I guarantee that things will work out more smoothly in your home.
As single persons, what do you expect in marriage? Your expectations shall not be cut off! Before my husband and I got married, we made discoveries from God’s Word that made us expect a hitch-free marriage. Till today, those expectations have not been cut off. If you expect the best, it will be yours!
A right expectation begins with being connected to God. You get connected by confessing your sins and accepting Jesus as your Saviour and Lord. That is what being born again is all about. If you are ready to be born again, please say this prayer:
Dear Lord, I come to You today. I am a sinner. Forgive me of my sins. Cleanse me with Your precious Blood. I accept You as my Lord and Saviour. Thank You for saving me. Now I know I am born again!
Congratulations! You are now born again! Till I come your way next time, please call or write, and share your testimonies with me through:
- E-mail: faithdavid@yahoo.com
- Tel. No: 234-1-7747546-8; 07026385437; 07094254102
Subscribe to:
Posts (Atom)