Na Robert E. Maziku
0653340950
Hakuna mtumishi yeyote anae furahia ukengeufu wa mtoto wake, kwa maana nyingine kila mtumishi hutamani familia yake imjue Mungu. Washirika huwaona watoto wa watumishi kuwa wana bahati kubwa sana kuzaliwa na wazazi wanao mfahamu Mungu. KATIKA MAKALA HII NIMETUMIA NENO MTOTO NIKIMAANISHA MZALIWA NA SIO KIGEZO CHA UMRI.
Wokovu
Nimchakato wa kuondolewa sehemu ya hatari kuelekea sehemu salama. Mfano mtu katekwa na maharamia wakati huo anakuwa hatarini sasa kinachofuata ni kutolewa hatarini ili awe salama, hapo anakuwa kaokolewa.
Yesu alikuja kutuokoa katika mazingira ya hatari(mikononi mwa Shetani), na kutuvuta kwake ambako ni salama. Kama mtu hajajua yuko hatarini huyo wakati mwingine huwa hapati msaada kwanza bali aoneshwe hio hatari aishuhudie mwenyewe kwanza, maana hata ukitaka kumuokoa atakimbilia hatarini zaidi akikukwepa wewe. Mfano nyumba inawaka moto na kuna mtu ukamuona yupo mlangoni nje ya hio nyumba inayo waka Moto halafu yeye hajui kama kuna hatari katika hio nyumba ukikurupuka kumkimbilia ukamtoe yeye anaweza kuufungua mlango na kuingia ndani kujificha akihisi una mkimbiza kwahio baada ya kumtoa kwenye hatari utakuwa umemuingiza hatarini zaidi.
WOKOVU HAURITHIWI
Kuna waumini wengi wanamtazamo wa Wokovu unaweza kurithishwa kwa watoto pengine hata baadhi ya watumishi. Mtoto kuzaliwa katika neema ya Wokovu haina maana ya kuwa atakuwa ameokoka lasivyo itakuwa anarithi dini sio Wokovu. Watoto wengi wa watumishi hawajaokoka kwasababu kihalisia hawajaiona hatari ya kuwa nje ya Yesu. Kwa mfano kama umeokoka nikikuuliza kwanini uliokoka? utakuwa unajibu zuri la kunipa sababu kuna namna ambayo ulikutana na Mungu wewe binafsi sio kwa kufata wazazi, ukiwafata wazazi ni sawa na kumsindikiza rafiki, ndugu, au wazazi kanisani akamuabudu Mungu au ukasikilize Neno wewe ili uamue kuokoka au la.
Kama mtu hajajua kihalisia utamu wa Yesu, Hasara ya kuwa kwa shetani na Faida zakuwa ndani ya Yesu utamlazimishaje aokoke kisa ni mtoto wa Mtumishi?. Huu ulazima hufanywa na watumishi kwa watoto wao kutokana na kutowapoteza washirika, maana wakiona mtoto wa Mchungaji haendi kanisani huonekana kama ni picha mbaya na mtoto huonekana kuwa msaliti kwa Mzazi au Wazazai. Wakati mwingine washirika wenyewe husababisha kwa kuwafata watoto hao binafsi na kuwalazimisha waokoke kwani ni aibu kwa wazazi.
MADHARA YA KUMLAZIMISHA MTOTO KWENDA KANISANI
Katika aya yangu ya tatu nimejaribu kuelezea maana ya kuokoka na nikaonesha madhara ya kutaka kumuokoa mtu ambae hajaona kama kuna hatari, Vivyo hivyo ukimlazimisha mtoto wa mtumishi kwenda kanisani ili asimuaibishe Mzazi wake utakuwa unamuweka hatarini yeye mtoto pia kanisa. Kwani atakachokwenda kukifanya humo ndani ni bora ungemuacha nje, Watoto wengi wa watumishi huenda kanisani kuchagua wasichana au kuficha maovu yao,na kwa watoto wakike wengi wao wanazalishwa kabla ya kuolewa. KAMA UNAHISI NAPOTOSHA FANYA UTAFITI KATIKA TAASISI AMBAZO WATOTO HAO WANAFANYA KAZI AU WANASOMA mwenendo wa maisha yao.
USHAURI
Mtoto wa mtumishi akifikisha umri wa mtu mzima kwa maana ya kuanzia miaka 18 aachwe achague mwenyewe kuwa anamtaka Yesu au hamtaki, ikumbukwe watu hawa huwa wako vizuri kimaandiko pengine hata maombi ingawa kimwili zaidi. Tangu anazaliwa alianza kusikia mapambio, maombi na kusikia mahubiri kitu ambacho huona haya mambo ni kawaida mnoo. WAACHWE WACHAGUE KUWA KWA SHETANI AU KWA YESU ILI WASIWE VUGU VUGU MAANA NI HATARI ZAIDI NDIO MAANA NIKASEMA UKIMLAZIMISHA UNAMSABABISHA AWE VUGUVUGU YAANI KOTE KOTE YUPO KWA MAANA NYINGINE UMEAMUA KUMSUKUMIA MOTONI ZAIDI.
NB:
NENO MTOTO LIMETUMIKA KAMA MZAWA AU MZALIWA NA SIO UMRI, HATA KAMA ANAMIAKA 40 ILA BABA YAKE NI MCHUNGAJI NIMEMUITA MTOTO NIKIMAANISHA MTOTO WA..
No comments:
Post a Comment