Baraka Nathan M'binhe
Producer wa Alfa One Love Production, Baraka Nathan M'binhe akiongea n Injili Forever Blog amesema ujio wa Video Production katika Muziki kwa ujumla unapelekea nyimbo zilizo katika mtindo wa audio kukosa thamani.Akijikita kwenye nyimbo za Injili anasema kwa sasa utakuta Albam yenye Video inauzwa 5000 Tsh wakati huo albam hio hio ikiwa katika Video itauzwa bei ile ile kwa vyovyote watu sasahivi wanasubili Video hawahitaji Audio sana wakati huo msanii asiyekuwa na fedha au mchanga atajikuta ametumia nguvu nyingi kwenye audio halafu mwisho wa siku hana milioni 2 au 3 za Video. Ushauri wake anaona afadhali Video zipande bei kwa mfano iwe 10000 halafu Audio ziwe 5000 ili angalau kuwe na sababu ya mtu kununua Audio lasivyo hakuna sababu ya Audio.
Akielezea changamoto nyingine katika Muziki huu wa Injili ni ghalama za radioni kupeleka nyimbo yako kupigwa kwa mfano, kuna radio unahitajika uwe na laki 2 nyimbo yako ili ipigwe tena hio haizid mwez mmoja. Sasa hio ni Radio moja sasa piga hesabu kuna radio ngapi Tanzania hata kama zingine zitakuwa bei ya chini bado msanii asiyekuwa na fedha mambo bado ni magumu kwao. Akijitolea yeye mwenyewe mfano anasema mpaka sasa ana CD kama mia ndani sababu ya ugumu wa kuitangaza kazi yake pia watu wanataka video ila akiitwa kwenye huduma akiimba watu wanaikubali kazi tatzo wanataka kuona video.
Mtazamo wake kuhusu uimbaji wa nyimbo za Injili baada ya miaka 5 ijayo ni waimbaji wenye fedha za kuweza kufanya Video, Promo kwenye Tv na Radio ndio watakuwa juu na sio uwezo wa kazi yao. Kuna watu wengi wanauwezo mkubwa kuliko hata ma super star ila vikwazo vimewafanya waishie kujitolea kuimba kwenye mikutano, semina na makanisani pasipo faida ya kiuchumi.
Alipo ulizwa kuhusu ushirikiano wa waimbaji wa Nyimbo za Injili alisema hakuna umoja kwa waimbaji wa Injili ndio maana hata collabo za Injili ni chache maana mahusiano sio mazuri kama wanao imba nyimbo za kidunia.
Mwamini Godfrey mmiliki wa studio ya Alfa One Love Production
No comments:
Post a Comment