Wednesday, January 29, 2014

Majaribu hutoka kwa Mungu na Shetani?

Amani ya Bwana iwe pamoja enyi nyote.

Majadiliano na fafanuzi ktk mada hii bila shaka yatatusaidia na kutupa ufahamu tuepuke kuwanung’unikia na kuwalalamikia Mungu na Wanadamu. Neno ‘’Majaribu’’ linaeleweka na kutumiwa na wengi hata limetungiwa nyimbo za Injli lakini nilipotafakari kwa uangalifu mambo ya Mungu na  tunavyolitumia neno ilo ktk maisha haya, nimelileta kama mada ili tupate ufahamu hasa kwenye swala la kufafanua ili kuweka utofauti wa wazi  kipi  ni hiki na  wala si kile, kwa maana iyo kupitia ninyi vyombo vya kazi vya Bwana, tunaweza pata akili, uelewa, ufunuo, Neno, Maandiko, fundisho, uzoefu, ushuhuda nk kwa ajili ya kusaidiana na kujengana Kikanisa/Kiroho na Kiimani.

Ili kuuingia Mjadala vema, unaweza tafakari  yasemwayo ktk Maandiko haya:

Kwa upande mmoja, Imeandikwa, furahini mnapoingia majaribuni-Yak.1:2, Wanafunzi walitishwa kutohubiri-Mdo.4:21,29,Stephano akapigwa mawe na kufa-Mdo.7:57-60, Mitume wanawekwa jela, wanapigwa na kuachiwa Mdo.5:16-42,Paul na Sila wakapigwa na kutupwa gerezani-Mdo.16:19-26,Petro anangojea kesho yake kuuawa baada ya mwenzake Yakobo kuchinjwa -Mdo.12:1-17, Ayubu anapoteza Watoto, Mali na Afya-Ayubu.1:14-19, 2:7, Mfalme Hezekia anaugua na Mungu anamwambia atakufa kisha akaomba, kifo kinafutwa-Isaya.38:1-4/ na 2Wafalme.20:1-4, Mtu ni kipofu toka kuzaliwa na ulemavu huo upo  kwa ajili kazi za Mungu kudhihirishwa ndani yake-Yoh.9:1-5, Ainea ameugua na amepooza miaka 8 pia  Dorcas mpendwa amekufa Petro anaomba, Ainea anapona na Dorcas anafufuka-Mdo.9:32-42, Mama Mkwe wa Petro amelala anaumwa homa, Yesu ana mgusa, anapona-Matt.8:14-15 

Kwa upande mwingine, imeandikwa kuwa duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu-Yoh.16:33, Je  tupate mema mkononi mwa Mungu nasi tusipate mabaya-Ayubu.2:10, jaribu halikuwapata ninyi isipokua lililo kawaida ya wanadamu-1Wakor.10:13. 

Kutokana na kichwa cha mada, nakigawa kupata Maswali makuu 4 ili kutoa mwelekeo mzuri unapojadili/changia, nayo ni haya:

Moja: Tukio/jambo gani  likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hili ni jaribu(test and trial, temptation)?

Mbili: Tukio/jambo gani  likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hiki ni kitu cha kawaida tu kwa wanadamu kwakua wanaishi duniani na kwamba tukiomba au tusiombe, tuko kiroho sana au kidogo, tumeokoka au bado, lazima yatatokea/tupata tu bila shaka? 

Tatu: Tukio/jambo gani  likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hili ni jaribu(test and trial) toka kwa Mungu lenye nia ya kutuimarisha au hili ni jaribu(temptation) la shetani kututoa kwa Mungu?

Nne: Au kuweka katika uhalisia, Mfano Ukifiwa na Mke, Mme, Mtoto, gari ikiibiwa, pinduka, ukavunjika mguu, ukiibiwa mali dukani, ukavamiwa na majambazi, ukipigwa sokoni wakati una hubiri au umekaa tu bila kuhubiri, ukakabwa na vibaka, ukiugua ugonjwa, kanisa-jengo likiunguzwa, ukikosa kazi muda mrefu, ukipata kazi lakini bosi akawa mnyanyasaji, Kanisa  kutokukua, huduma kudumaa, kutopandishwa cheo,kukosa pesa,kutoweza kujikimu kwa utele mahitaji ya maisha, kuchelewa kuoa/kuolewa, kutopata mtoto, kua tasa nk, yapi kati ya hayo ni majaribu toka kwa Mungu, Shetani  au ni  mambo ya  asili au kawaida tu ktk maisha duniani hapa?

Press on,

Edwin Seleli


SOURCE: STRICTLY GOSPEL

No comments:

Post a Comment