Friday, November 8, 2013

BAHATI BUKUKU AFIWA NA BABA YAKE

WAIMBAJI WAJITOKEZA KUMFARIJI BAHATI BUKUKU MSIBA WA BABA YAKE


Hizi ni baadhi ya picha za msiba wa baba mzazi wa mwimbaji gospel nchini Bahati Bukuku aitwaye mzee Lwaga Bukuku ambaye alifariki dunia hivi majuzi jijini Dar es salaam. ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwa mwimbaji huyo maeneo ya Tabata, watu mbalimbali wakiwemo waimbaji wenzake Bahati kama Jennifer Mgendi, Christina Shusho, Christina Matai, Neema Gasper na wengine walifika nyumbani hapo kumpa pole, mwili umesafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa mazishi.





Msiba nyumbani kwa Bahati.


Bahati akiwa na wafiwa wengine.



Baadhi ya waimbaji wakiongozwa na Christina Shusho wakiwa msibani hapo.



Neema Gasper akimsifu Mungu huku akipewa nguvu na mwana GK Silas Mbise.


Silas Mbise akilonga huku Joshua Makondeko akifurahia maneno ya busara kutoka kwa kijana.


Bahati akizungumza jambo.


Solomon Mukubwa akiimba msibani hapo.


Beatrice Mwaipaja akiimba.


Jeneza lenye mwili wa marehemu mzee Lwaga Bukuku.



Mchungaji akiongoza ibada ya mazishi.


Bahati Bukuku akiwa na wafiwa wengine wakati wa ibada ya kuuaga mwili.


Hata hivyo alamanusura mambo yaende kombo, ambapo utata ulijitokeza wapi mwili uzikwe, kati ya Mbeya ama jijini Dar eneo la Sinza, ambapo kaburi lilichakuwa limeandaliwa, tofauti na mipango mingine ilivyokuwa.

Tukio hilo ambalo limeshuhudiwa na Gospel Kitaa, lilianza kufukuta pale ambapo ilitangazwa kuwa marehemu Lwaga Bukuku angezikwa Mbeya, jambo ambalo lilizua taharuki kwa baadhi ya wafiwa ikiwemo watoto, ambapo baadhi waligoma kuaga mwili – huku kaburi lililokuwa limeandaliwa maeneo ya Sinza, likibaki tupu bila kujua nini kinafuata.

Licha ya juhudi za baadhi ya watu kujaribu kuweka mambo sawa, bado haikuwa rahisi kueleweka kwa maamuzi yaliyofanywa, ambapo hadi GK inaondoka eneo la tukio, mwili ulisafirishwa kuelekea Mbeya.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
chanzo ni www.gospelkitaa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment