Wednesday, October 30, 2013

AMANI



Kuna makundi mawili ya Amani: nayo ni

(A) Amani itokanayo na ulimwengu

(B) Amani itokanayo na Yesu Kristo.(Amani ya Kristo)

YOHANA 14:27 > Amani nawaachieni, Amani yangu nawapa, niwapavyo mimi sivyo ulimwengu utoavyo.

Ukiangalia kwa Makini katika Mstari huu utagundua kwamba Yesu anatoa Amani, na ulimwengu nao unatoa Amani, lakini Amani hizi ni tofauti kabisa.

Atupavyo Yesu, sivyo Ulimwengu utoavyo.

Maanayake ni kwamba : Amani aitoayo Yesu siyo kama Amani itolewayo na ulimwengu huu.

Ifuatayo ni tofautu baina ya makundi haya mawili ya Aman

(A)= Amani itokanayo na Ulimwengu.

Kuna aina mbili za Amani zitokanazo na Ulimwengu

1, Amani ya binaadamu iliyo sawa na njia za ulimwengu

2, Amani ya shetani mkuu wa ulimwengu

1- AMANANI YA KIBINAADAMU ILIYO SAWA NA NJIA ZA ULIMWENGU

Biblia inatuambia kwamba hatupaswi kuifuata Amani ya namna hii ya kibinaadamu

TORATI 23:6 = usifuate Amani yao, wala heri ya siku zako zote, milele

Amani ya kibinaadamu ni Amani anayokuwanayo mtu kutokana na kupenda kitu anacho chagua kukifanya au kukitenda kutokana na njia za kawaida za ulimwengu

Mtu yeyote anaweza kuwanayo Amani hii hata kama haja okoka

Mfano -:
Mtu amekaa muda mlefu bila kazi, na akaletewa taharifa ya nafasi ya kazi mahari furani , mtu yeyote katika mazingira hayo ni lazima atakuwa mwenye Amani, na atakwenda haraka kwenye kazi hiyo. Hii ni amani ya kawaida kwa kila mtu wa ulimwengu huu

=Mtu aliyekosa kitu furani kwa muda mlefu, akija kupata kitu hicho ni lazima atakuwa mwenye Amani

=Mtu akipata mchumba anaye mpenda, ni lazima atakuwa ni mwenye Amani

=Wanandoa waliotafuta mtoto kwa muda mrefu , siku wakipata mtoto ni lazima watakuwa wenye Amani

=Mlevi mwenye kiu, au hamu ya Pombe, akipata pombe ni lazima atakuwa mwenye Amani, kadharika na mtu wa sigara naye vivyn hivyo.

Hizi zote ni amani za kawaida zitokanazo na ulimwengu huu.

2= Aman ya shetani mkuu wa ulimwengu.

Hii ni Amani anayokuwa nayo mtu anayeishi katika dhambi, anafanya dhambi na kuenenda kinyume na Neno la Mungu lakini yeye anaitetea dhambi hiyo na kusema yeye ana Amani katika kuifanya dhambi hiyo, na hii sio Amani ya Kristo

2WAFALME 9:22 = ikawa Yoramu alipomuona Yehu, akasema, Je, ni Amani yehu? Akajibu, Amani gani maadamu uzinzi wa mama yako Yezeberi na Uchawi wake ni mwingi?

TORATI 29:19-21 = ikiwa msikiapo maneno ya laana hii, ajibarikiye mtu huyo moyoni mwake na kusema nitakuwa katika Amani nijapotenda katika upote wa moyo wangu kwa kuziangamiza mbichi na kavu, Bwana hata msamehe mtu huyo, lakini wakati hasira ya Bwana na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itakuwa juu yake, na Bwana atalifuta jina lake chini ya mbingu......

MITHALI 23:20 = Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo

mtu mlevi huwa na amani moyoni mwake, na Amani hiyo ni amani itokanayo na mkuu wa pepo (ibilisi) kwamaana maandiko yanasema ,, Walevi hawataurithi ufalme wa mbinguni =1wakoritho 6:9-10,

Amani ya shetani ni kuona mtu anaishi maisha ya dhambi siku zote za maisha yake hapa duniani,

(B) AMANI ITOKANAYO NA KRISTO (Amani ya Kristo)

=Amani ya Kristo inayoamua mioyoni mwetu hupatikana ndani ya Kristo, Maana yake ni kwamba, Amani ya Kristo hupatikana katika Utakatifu wa Kristo
=Katika mapenzi yake,
=katika Neno lake,
=katika mpango wa Mungu

YOHANA 16:33a =Hayo nimewaambia mpate kuwa na Amani ndani yangu.

AMANI yeyote ambayo siyo Amani ndani ya Yesu, hiyo ni Amani ya Ulimwengu.
Amani ndani ya Yesu ni Amani ndani ya Neno la Mungu, Yesu Kristo ndiye Neno (YOHANA 1:1-)

Amani yeyote iliyo nje ya Neno la Mungu hiyo ni Amani ya shetani mkuu wa ulimwengu.

Amani ya Kristo ni ile inayopatikana baada ya kumuomba Mungu juu ya jambo furani na kupokea kile ulichotarajia kupokea.

MUNGU AKUBARIKI

 .. .usikose SOMO lijalo, litakuwa na kichwa cha habari kiitwacho ,,IMANI,, ahsante.

No comments:

Post a Comment