Wednesday, October 16, 2013

APOSTLE ELIYA SIMONI: SOMO LA IMANI

                                                             Apostle Eliya Simon-0759 166 934



                                         IMANI

YALIYOMO
            1. Utangulizi
            2. Fomula
            3. Hitimisho

DHUMUNI
-Kujua namna ya kuishi kwa Imani –Warumi 1:17c
-Tumpendeze Mungu kwa Imani—Waebrania 11:6

ANDIKO KUU –Warumi 10:17- Basi Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la kristo ”

1.UTANGULIZI
-Wakristo wengi hawajapata kuelezwa kwa usahihi somo hili la Imani, ndio maana nimelipa kipaumbele. Najua utajifunza kitu, twende hatua kwa hatua.

2.FOMULA
-Kutoka katika andiko letu kuu la Warumi 10:17, tunaweza kutengeneza FOMULA rahisi ambayo itatusaidia kuelewa IMANI kwa urahisi;

          IMANI = KUSIKIA + NENO(la Kristo)

-Tumepata vitu vitatu katika fomula yetu, 1.NENO, 2.KUSIKIA, na 3.IMANI ambayo ni tokeo, nitaelezea kila kipengele ili tuielewe FOMULA yetu rahisi;

1.NENO(la Kristo)
Kwa lugha asilia ya Agano Jipya,yaani kigiriki, neno NENO lina maana mbili,
          (a) LOGOS   na  (b) RHEMA
LOGOS – Ni Neno ambalo halibadiriki, au ni Neno lililoandikwa, au ni taratibu zinazoendesha jambo fulani bila kubadirika.
Mfano mzuri wa Logosi ni Biblia, pia ni taratibu zote zinazoshikiria taratibu za ulimwengu na mbingu. ZABURI  119:89

RHEMA – Ni neno maalum, kwa watu maalum, kwa wakati maalum, katika mazingira maalum na katika hali maalum. MATHAYO  4:4- ‘….kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu’, ni Mungu anaongea wakati uliopo(sasa), tarehe ya leo. Ahadi zote za Biblia utazipokea ikiwa Yesu atazibadiri kutoka Logos nakuwa Rhema kwako.

-Sasa tujiulize, Mtume Paulo alitumia neno gain kati ya hayo mawili, jibu ni RHEMA.
Sasa tuboreshe Fomula yetu rahisi;

          IMANI = KUSIKIA + RHEMA

2.KUSIKIA
-Hili neno KUSIKIA ni mjumulisho wa maneno kadhaa, ambayo ni;
          -maono, ndoto, kusikia rohoni,kuona vya rohoni na kutambua mambo ya rohoni.
JOELI 2:28-30, Warumi 8:14a, Ufunuo 1:10-11,

-Sasa ili mwanadamu asikie/aone ni lazima Mungu azungumze/aonyeshe, Mungu huzungumza kwa namna nyingi lakini njia ambayo ni bora kuliko zote ni njia ya YESU kwakupitia ROHO MTAKATIFU, soma WAEBRANIA 1:1-2. Kitendo cha Mungu kuongea na mwanadamu ki-Theolojia kinaitwa DISPENSATION.

Toka agano la kale mpaka jipya kuna dispensation nne,yaani Mungu amekuwa akiongea na Mwanadamu kwa njia 4. Katika njia zote nne(4) za Mungu kuongea, kigezo ni kimoja tu, KUSIKIA KWA BIDII,--Kumbukumbu La Torati 28:1, YOHANA 10:3,16,27

3.IMANI
-WAEBRANIA 11:1
Kwa kifupi tungesema Imani ni kutarajia kitu ULICHOSIKIA/KIONA. Lugha ya kiingereza ina maneno mawili ambayo ni BELIEVE na FAITH, ambayo Kiswahili tunapata neno moja tu la IMANI.

-BELIEVE(Imani muitikio) – Ni neno aina ya NOMINO, lakini FAITH (imani utendaji)– Ni neno aina ya KITENZI. Maana yake unapoamini bila kuchukua hatua ndo inaitwa BELIEVE, lakini unapoamini na kuchukua hatua ndo inaitwa FAITH.Tuangalie mfano wa NUHU;
          MWANZO 6:13-14, Mungu anaongea na Nuhu,anamwambia mwisho wa Dunia umefika,kwahiyo atengeneze Safina. Kitendo cha Nuhu kusikia na kuamini kuwa itatokea ndo inaitwa BELIEVE, Nuhu anapoanza kuchukua hatua ya kutengeneza Safina ndo inaitwa FAITH. Mara nyingi Biblia inapozungumzia Imani inamaanisha FAITH,yaani Imani katika Utendaji. Pia soma MWANZO 15:4-6, WAEBRANIA 11:7-10.
-Pia Imani ni Tunda mojawapo la ROHO MTAKATIFU, wakati mwingine huwa inaitwa Imani ya Mungu—MARKO 11:22

KWA KIFUPI—Unapotaka kuwa na Imani sahihi, ni lazima usikie kwa masikio yako ya kiroho, au uone maono kwa macho ya Rohoni, au uote ndoto kwa utu wa ndani kutoka kwa Yesu kwa kupitia Roho Mt. Mchakato wa Imani unaanzia ndani(rohoni) kisha unakuja nnje(mwilini), ndiomaana wengi wameshindwa.

3.HITIMISHO
Fuata hizi hatua sita(6) kudhilisha Imani yako
          a)Tamani/omba Mungu akupe NENO—Isaya 44:3, Mathayo 7:11
          b)Tarajia KUSIKIA—Danieli 2:17-19, Habakuki 2:1-2
          c)Amini(believe) uliyo YASIKIA—Mwanzo 15:6
          d)Fanya(Faith)uliyo YASIKIA —Yohana 14:12
          e)Kiri/tamka Imani yako—Warumi 10:10b
          f)Mungu atakudhihilisha—Yeremia 1:12, Isaya 55:11


No comments:

Post a Comment