Saturday, October 12, 2013

MAMBO MANNE(4) YALIYOPOTOSHWA NA VIONGOZI WA DINI NI HAYA.




Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

BWANA YESU asifiwe wapendwa wangu wote, namshukuru sana MUNGU kwa uzima na pia nashukuru sana kwa ujumbe wa pongezi kwa kazi ya MUNGU.
Leo nakuletea somo hili nikigusia mambo ambayo yamepotoshwa kwenye dini mbalimbali na madhehebu pia.  Mambo haya huwafanya watu watende dhambi na wasienende kwa roho jambo ambalo ni hatari sana kwa waenda mbinguni.

MAMBO YALIYOPOTOSHWA NA VIONGOZI WA DINI NI HAYA:

1:   Maombi kwa ajili ya wafu.
 viongozi wengi hufundisha kwamba hakuna kuokoka duniani na hao hao   mtu akifa wanamwombea kwamba alazwe pema peponi kana kwamba kuna wokovu baada ya kufa. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu.(Waebrania 9:27).
-Ndugu zangu hakuna mtumishi, mchungaji, nabii, padri au askofu aliye mkweli kuliko neno la MUNGU. Sasa hizi habari za kuombea wafu tena wafu wengine ambao ni maarufu au viongozi wa serikali huombewa kila mwaka ili wahamie pema peponi. Hii ni kujidanganya  na kujifariji ubatili.
-Kanisa haliwezi kuomba mfu kupumzika kwa amani pema peponi, Ndugu zangu wakati wa wokovu ni sasa hivyo baada ya kufa ni hukumu. Watakie kupumzika kwa amani wafu ila tambua kwamba huwezi kuwabadilishia makao yao ya milele, kama ni mbinguni ni mbinguni tu na kama ni motoni ni motoni tu.
*Kuombea wafu huwafanya wenye dhambi kuendelea kutenda dhambi wakiamini kwamba baada ya kufa kanisa litaomba ili wao waingie mbinguni. Ndugu nakuambia tena WOKOVU NI SASA.
Katika Luka 16:26…
Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'' Biblia inatuonyesha watu waliokufa  wengine wako pema peponi na wengine wako kuzimu,’’  ’’
MUNGU humpokea mwenye dhambi ambaye hutubu kwa woyo na kujitakasa kwa msingi wa imani peke yake katika damu ya YESU KRISTO. Hivyo humpa uzima wa milele. 2 Kor 6:2’’
(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)   ‘’
Wakati wa wokovu ni sasa
Wakati wa kuokolewa/kuokoka ni sasa
Wakati huu ndio unatakiwa kuokolewa sio baada ya kufa.

2: Kutenda mema uwezavyo.
BWANA YESU katika Yohana 16:9 anasema  ‘’Kwa habari ya dhambi kwa sababu hawakuniamini mimi’’
Kumbe unaweza ukatenda mema lakini kama huna YESU hakika utaangamia
Binadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa MUNGU. Warumi 3:23.
Huu mwili ni wa dhambi na pia unarithi dhambi hivyo ni nguma sana kwa mtu yeyote kutenda mema tu bila kutenda dhambi, na katika Historia ni BWANA YESU KRISTO peke yake ambaye aliishi duniani zaidi ya miaka 30 bila kutenda dhambi hata moja.Ndugu yangu unaweza kutenda mema yote unayoyafahamu lakini bila kumpa BWANA YESU maisha yako hakika huwezi kuingia katika ufalme wa MUNGU. NDUGU KUOKOKA NI LAZIMA KAMA UNATAKA KWENDA UZIMA WA MILELE.

3:Kushika amri.
Unaweza ukadhani kushika amri peke yake ndio tumaini lako. Kushika amri hakutatoa uzima wa milele.
Unaweza kuwa hutaji bure jina la MUNGU, huibi,hui,huzini, unashika sabato ya kiyahudi lakini kama Humkubali YESU kwa BWANA  na MWOKOZI wa maisha yako ni kazi bure. Wagalatia 3:21-22.''
Basi je! Torati haipatani na ahadi za MUNGU? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria. Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya YESU KRISTO.'' 
pia Wakolosai 2:20-23,Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Uzima wa milele unapatikana kwa imani kwa YESU KRISTO pekee.
Shika yote lakini kama YESU KRISTO hayuko moyoni mwako ni kazi bure.Ndugu WOKOVU NI SASA.

4:Upatanisho/ Uombezi.
Eti watakatifu mbinguni hutuombea au wanaweza kutupatanisha na MUNGU mfano Bikra Mariamu, Petro mtakatifu au Yusufu mtakatifu.
Hao hawawezi kufanya lolote juu ya mtu mwenye dhambi kwani Wokovu haukutimizwa kwa hao ila kwa YESU KRISTO. Matendo 4:12.

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. 
 Hata ushirika watu wanaupotoka lakini nakuambia Dini  yeyote ya kikristo bila KRISTO mwenyewe ni Ubatili.
Ndugu zangu Hii ndio saa ya Wokovu, hivyo kama hujampatia BWANA YESU KRISTO maisha yako basi nafasi ya kufanya hivyo ni leo.
Omba maombi hata mafupi na utaokoka kisha acha dhambi zote na tafuta kanisa la kiroho.

Sema
‘’BWANA YESU, niko mbele zako mimi ni mwenye dhambi, lakini leo naamua kukufuata wewe BWANA YESU, Natubu dhambi zangu zote, ninazokumbuka na nisizozikumbuka, Futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike jina langu kwenye kitabu cha uzima, tangu leo nimeoka, naufunga ukurasa wa dhambi na kuanzia sasa ninafungua ukurasa wa kumcha MUNGU nikiwa ndani yako BWANA YESU. Nipe ROHO MTAKATIFU ili aniongoze kuanzia sasa. Asante BWANA YESU kwa kuniokoka, niongoze BWANA na niwe mbali na kuonewa kuanzia sasa, navunja maagano yote ya shetani niliyoingia, najitenga na laaza za ukoo na roho za mizimu katika jina la YESU KRISTO, nishindia vyote BWANA. Katika jina lako takatifu BWANA YESU nimeomba, nimeamini na nimepokea. AMEN’’
Baada ya maombi haya Tafuta kanisa la kiroho wanapohubiri kweli ya MUNGU na wanakiri  WOKOVU tena wanaikemea dhambi hadharani, waeleze na watakuombea na kukuongoza kisha utaukulia Wokovu wa BWANA YESU pamoja na washirika wengine.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika KRISTO.
Peter Michael Mabula
(Maisha ya ushindi Ministry)

No comments:

Post a Comment