Tuesday, October 15, 2013

EUBERT ANGEL





   NABII EUBERT ANGEL

 NABII KIJANA ALIYE TABIRI UVAMIZI WA WESTGATE MALL JIJINI NAIROBI.

Nabii Uebert Angel ni Rais wa huduma ijulikanayo kama Spirit Embassy akiamini muanzilishi ni Yesu Kristo(yeye ni Rais, Yesu Kristo ni Mwanzilishi). Jina lake limekuwa maarufu kwa miujiza, uponyaji, Ishara, Maajabu na Unabii unao timilika kwa wakati husika. Kati ya matukio yalio gumzo nchini Zimbabwe na watazamaji wa Runinga ya Miracle TV ni Unabii alioutoa tarehe 23 septemba 2012 siku ya jumapili katika ibaada ya moja kwa moja kupitia Miracle TV kuhusu mlipuko Nairobi.

Alisema "This is an open space...like you can go there and do your market there, and this is a bomb coming up there". Cha ajabu alisema wazi kuwa shambulio hilo haliepukiki(halizuiliki).

Tarehe 30 juni 2013 alirudia tena "We need to really pray for Kenya he said, There's a lot of progress happening in Kenya, but this is a small group that decided the christian community is going up too much, lets kill some people. I say even police, an authority where even guards are there and they are bombing."

Tarehe 21 julai 2013 akasema tena. "Remember the Kenya prophecy?. These are days closing, they are coming close and coming close." na akawasisitiza kuanza mfungo wa kanisa zima kuanzia jumatano mpaka tarehe 21 mwezi wa nane 2013. Hatmae tarehe 21 mwezi wa tisa 2013 unabii ukatimia.

Eubert Angel amezaliwa 6/9/1978 takribani miaka 35 iliyopita.

IMEANDIKWA NA ROBERT MAZIKU 0653340950.

No comments:

Post a Comment