Wednesday, October 23, 2013

YESU SI MBUZI -- 2



c) Kuzaliwa Kwa Maji na Roho Mtakatifu

Yohana 3:5, Tito 3:5, Ebrania 10:22, 1 Yohana 5:6,9, Mdo 10:44-48, Hapa ndipo penye siri yote, wengi wanasema tumeshabatizwa kwahiyo hakuna jipya, soma MDO 8:12-17 utawaona wenzako walivyopungukiwa na kitu cha muhimu-----ROHO MT………..….
………………………………..ENDELEA…………………………….
Hapa nitaelezea kwa umakini zaidi, naomba hiki kipengele nikiite MASHAHIDI WATATU, nikimaanisha ROHO MT, MAJI na DAMU --- 1 Yohana 5:6
- Hawa mashahidi watatu ndio wanaotengeneza AGANO JIPYA, labda tujiulize swali, Agano Jipya lilifanyika mto jordani au kalvali, najua wapendw wengi wangejibu kalvali (msalabani), sio kweli. Tunaposema Agano Jipya tunamaanisha Mungu ANACHUKUA DHAMBI(MAJI), kisha anatupa ROHO MT, hili ndilo Agano Jipya. Sasa Damu inakazi gain ? Damu ni USHAHIDI wa Agano lililofanya,kwahiyo Damu yenyewe sio Agano, bali ni KIASHIRIA cha Agano, ni kama vile PETE kwa wanandoa. Ndio maana ROHO MT na MAJI vimetajwa pamoja mara nyingi, na Biblia inapotaja Maji na Damu bila kutaja ROHO MT inajua kwamba ndani ya Maji kuna mgao wa ROHO MT.  ---kutoka 24:7-8, Waebrania 9:16-20
- Naomba niseme hivi, hata ukifunga,ukikesha,uki omba miaka 100 kwa ajili ya kupokea Roho Mt, HUTAPOKEA !!!,kinachofanya mtu apokee Roho Mt ni ile hali yakutokuwa na DHAMBI YA ULIMWENGU ndani ya Moyo wa mwanadamu, na ndio maana tukio la Ubatizo limekuwa likiendana na kupokea Roho Mt,sio Maombi. Haya matukio mawili siku zote yapo sambamba, Mfano;Yesu aliona udhihilisho wa Roho Mt alipomaliza kubatizwa –Mathayo 3:16, Mtume Paulo---ubatizo na kupokea Roho Mt vilienda pamoja—Mdo 9:17-18, soma hapa uone Petro anavyowashauri wanadamu –Mdo 2:38.Kitabu chote cha Matendo ya mitume kimejaa matukio haya mawili---KUMKABIDHI MUNGU DHAMBI na MUNGU KUTOA ROHO MT.
- Wachungaji wengi wamewaaminisha washirika wao kuwa wana Roho Mt, huo ni uongo,swala la kuwa na Roho Mt sio la Imani, ni uzoefu(you have to experience it), lazima kuwe na dalili, alama zinazoonyesha kuwa wewe una Roho ---ukisoma Efeso 1:13—utagundua Roho Mt ndiye anayempiga mtu MUHURI kuwa amesamehewa Dhambi kwa Maji. Dalili mojawapo rahisi ya kujua mtu amepigwa muhuri ni KUNENA KWA LUGHA---Mdo 10:45-46 – Mungu alimgonga Ibrahimu muhuri kwa namna gani ?--- Kutahiliwa, unaona, nilazima dalili zionekane. Unapojaribu kunena kwa Lugha bila kuongozwa na Roho Mt, utakuwa unafungua njia ya mapepo kukujia.
- Njia sahihi ya kumpokea Roho Mt; Tambua kuwa Mungu anataka aweke Agano na wewe, Agano hilo wewe unatakiwa umkabidhi dhambi zako zote, Mungu atazichukua zote na anakupa zawadi ya Roho Mt. Sasa amini kuwa makabidhiano ya dhambi zako yalifanyika kwa maji, na Yesu akakubali kuzichukua zote kwa kuwekewa mikono na Yohana na kuingia ndani ya maji, ukisha amini hivi nenda ukabatizwe, Mungu atakupa zawadi ya Roho Mt ambaye ndiye anawajibika kukutunza mpaka Yesu atakaporudi tena, baada ya hapo Mungu ataanza kukutazama wewe kwa miwani ya Damu ya Yesu, hatakuhesabia dhambi tena.
3. ONGEZA MTAZAMO
Mathayo 3:11 ‘..…atawabatiza kwa Roho Mt na kwa Moto ’.
a) Ubatizo wa Roho Mt
 Yohana anaongea vitu ambavyo kila mwanadamu angepaswa avitafute sana, kwasababu ndio Agano Jipya. Naomba niseme kwamba Mungu hana mpango na mtu yeyote aliye nnje ya Agano, ili ubatizo wa Roho Mt ufanikiwe inapaswa mtu aamini ondoleo la dhambi na pia awepo mtumishi aliyejaa Roho Mt, hautapokea Roho Mt mpaka yeye anayekuongoza kupokea Roho Mt awe ametiwa muhuri na Yesu,kwasababu jukumu la kubatiza kwa Roho Mt nila Yesu. Kwahiyo sio kila mchungaji anaweza kukufanyia mchakato wa kujazwa na Roho Mt. Soma Mdo 19:1-6 – utaona watu wa Efeso walikuwa wamebatizwa ubatizo wa Yohan lakini hawakuwa na Roho Mt, kwamba aliyewabatiza hakuweza kuwawezesha wapate Roho Mt. Soma pia Mdo 8:12-17 – Samaria walibatizwa lakini hawakupokea Roho Mt mpaka alipokwenda Petro na Yohana. Nataka niseme nini hapa !! imani yako lazima iendane na tendo la kuoshwa lakini ni lazima awepo mtumishi sahihi wakuyafanya hayo yote yawe na maana
b) Ubatizo wa Moto
-Kubatizwa kwa Moto ni kitendo cha Yesu kutufanya sisi tuwe harufu nzuri kwa Mungu, yaani atufurahie—2 korintho 2:14-15, sisi tuliozaliwa mara ya pili ni SADAKA ya kuteketezwa kwa moto, sasa Yesu akiwa kama kuhani anatuchukua sisi na kututeketeza kwa moto ili kumletea Mungu harufu nzuri. Soma Mwanzo 8:20-21, kutoka 29:18, Hesabu 15:3, Kwahiyo Yesu anatutoa kwa Mungu kama sadaka ya kuteketezwa, namaanisha Yesu anatuteketeza kwa Roho Mt. Hili ndilo Agano Jipya, yeyote ambaye hataelewa hapa atakuwa ameukosa ufalme wa Mungu (hataingia mbinguni). Yesu atakapokuja atawanyakuwa wale wenye Roho Mt tu !! Nakusihi sana msomaji wangu, fanya uwezavyo umpate Roho Mt kwasababu AHADI KUU ya Mungu kwa mwanadamu ni Roho Mt, nnje na hapo ni makida-makida
c) Watumishi Feki
- Hawa niwatumishi wanaoanza huduma bila ya luksa ya Yesu(Roho Mt)—Mdo 13:2, wamesababisha madhara makubwa sana kwasababu Mungu haitaji watu wakujitolea kumtumikia, na ndio maana mtembeo wa Roho Mt kwa watumishi wengi sio mzuri, mimi kama mtumishi mmojawapo naomba nikubali hili kosa. Utumishi ambao Roho Mt hajauanzisha, kamwe hatautimiza, samahani kwa kusema hivi;-mkristo ambaye hana Roho Mt, SIO MWANA WA MUNGU.
4. HITIMISHO
-Soma kwa umakini hapa, Agano la Mungu na Wanadamu toka mwanzo na mpaka mwisho wa ulimwengu ni hili, “MIMI NITAKUWA MUNGU WENU, NANYI MTAKUWA WATU WANGU---Ezekiel 36:25-29”, sasa basi, kikwazo kikubwa cha hili Agano kuwepo ni DHAMBI YA ULIMWENGU, sasa Mungu akawa anatafuta namna ya kuiondoa hii Dhambi moja kwa moja ili ATIE ROHO YAKE ndani yetu. Uwepo wa Roho Mt katika maisha ya mtu ndo yanaonyesha mafanikio ya Agano kwasababu Roho hakai sehemu chafu.
- Kwahiyo Yesu amefuta dhambi kwa Maji, Roho Mt akapata nafasi ya kuja Duniani, na Mungu akalinyunyizia hilo Agano kwa DAMU,pale msalabani. Kila wakati Mungu anapotaka amtazame mwanadamu,kwanza ni lazima avae MIWANI (aitazame damu msalabani) ndio amtazame, ndio maana hatatuhesabia hatia tena kwasababu HAIONI, anaona Damu-Damu tu.
-Agano la kale Mungu alishindwa kugawa Roho Mt kwa wote kwasababu dhambi za watu zilikuwa zinafunikwa tu bila kufutwa, lakini agano Jipya kila mtu anayo haki ya kupata Roho Mt kama vigezo na mashart yakizingatiwa
-Yesu sio Mbuzi ila amechukua uhusika wa Mbuzi wa Agano la kale, YESU NI MWANA WA MUNGU, YESU NI BWANA, YESU NI ALFA NA OMEGA,YESU NI MFALME ATATAWALA MILELE YOTE……………………………AMENI……………………………

No comments:

Post a Comment