TOFAUTI KATI YA SERIKALI YA MBINGUNI NA DUNIANI (sehemu ya 2)
Na Mwinjilist i Gerald Robert
JE SERIKALI ZA DUNIANI ZITAWEZA KUWA NA AMANI YA KUDUMU ?
Serikali za Duniani zinaoneka wazi wazi kwamba zimeshindwa kupata Amani ya Moja kwa moja (Amani ya kudumu) japokuwa zimekuwa zikiitafuta Amani hiyo kwa gharama kubwa ya pesa kwaajili ya kuunda vikosi vya kijeshi vya kutafuta Amani, au kuilinda Amani lakini bila yakuwa na mafanikio yoyote
Upatikanaji wa Amani kwa serikali za kidunia unakwamishwa na mambo mengi sana, zifutazo ni baadhi ya sababu
1= Viongozi wa Serikali za kidunia hawapendi kuondoka madarakani kwasababu wao hupenda sana kutumikiwa na sio kutumika kwaajili ya Raia au watu wanao watawala katika utawala wao
Yesu Kristo alipokuja Duniani alileta mfano mzuri sana ambao kama viongozi hawa wa kidunia wangeukubali mfano wa Uongozi wake, leo hii Dunia ingekuwa ni sehemu ya Amani na Salama
MARKO 10:45 = kwamaana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa bali kutumika na kutoa nafsi iwe faida kwa wengine.
2= Utawala wa nchi, Imani za wananchi juu ya mafundisho ya Mungu,
kuna baadhi ya nchi, au Watawala wamekuwa wakitawala kwa kufuata sheria za Dini, na ikumbukwe kwamba sheria za Dini huwekwa na wanadamu ambao ni washika Dini na kuna wakati sheria hizo za Kidini hupingana na sheria za Mungu, mwanadamu anapoenenda kinyume na sheria za Mungu hapo ndipo matatizo yanapoanzia (Kumbukumbu la Torati 28:15-64-)
Sasa tuangalie mfano namna Mungu anavyo penda tuishi kwa kumtii yeye
Mfano ;--
WARUMI 12:17-21, (Hii ni sura kutoka Kitabu cha Biblia Takatifu) inasema hivi.
,, Msimlipe mtu Ovu kwa Ovu, angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote, kama ya mkini, kwa upande wenu, Mkae katika Amani na watu wote,
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa, anena Bwana,
Lakini Adui yako akiwa na njaa, mlishe, akiwa na kiuu, mnyweshe, maaana ufanyapa hivyo unampalia makaa ya moto kichwani pake,
Usishindwe na Ubaya, bali Uushinde ubaya kwa wema. (mwisho wa kunukuu)
Hapo tumejionea jinsi mifano hiyo miwili inavyopingana katika katika kupata Amani ya kudumu kwa serikali za duniani
AMANI ITOKAYO JUU MBINGUNI
Dunia nzima ingeweza kuwa na Amani kama watu wote tungekuwa na Upendo wa kweli bila ya kulipizana visasi, na kung'ang'ania Madaraka
YOHANA 14:27
Amani nawaachieni, amani yangu nawapa, niwapavyo mimi sivyo ulimwengu utoavyo. . . .
Hapa tunaona kwamba, Yesu Kristo kabla ya kuondoka duniani alituachia Amani, na Amani hiyo siyo kama Amani ile ambayo inatolowa na ulimwengu huu kwa kupitia Watawala wa serikali za kidunia.
Kwenye upendo hapo ndipo Amani inapo patikana
YOHANA 13:34
Amri mpya nawapa, Mpendane, kama nilivyo wapenda ninyi, nanyi Mpendane vivyo hivyo.
Kwakuwa Mungu alifahamu kwamba wanadamu tu dhaifu kwa asili yetu. Akatuwekea Amri
YOHANA 15:17
Haya, nawaamuru ninyi mpate kupendana (rejea Yohana 14:34)
Neno ,,Amuru,, maana yake ni Lazima, sio Ombi,
kwahiyo Upendo sio jambo la hiyari, bali ni Amri kutoka kwa Mungu, ukiidharau Amri ya Mungu, yapo madhara yakayokupata kwa kudharau kwako.
WARUMI 13:10
Pendo halimfanyi jirani Neno baya, basi, pendo ndilo utimilifu wa sheria (ya Mungu)
kwahiyo kutokuwa na upendo baina ya mtu na mtu, au nchi na nchi, hapo ndipo Amani hutoweka, kwamaana Upendo hauhesabu mabaya. ( 1wakorinto 13:4-8)
AMANI ITABAKI KWA WATAKATIFU WA MUNGU
ZABURI 16:3
Watakatifu waliopo Duniani ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao.
Mungu akipendezwa na wewe hawezi mabya yaje kwako, (hata kama ukifikwa na mabaya ni lazima utayashinda) hivyo sikuzote wewe utakuwa ni mwenye Amani, kwakuwa uwepo wa utakuwa pamoja nawe daima ni kwakuwa Mungu hapendezwi na waovu.
Hata kama nchi itafikwa na mabaya lakini watu wa Mungu (watakatifu) wao wataendelea kuishi na kuwa na Amani hiyo ni kwakuwa Watakatifu wa Mungu hawaishi kwa kuitegemea sana Amani ya ulimwengu huu bali huishi kwa kulitegemea Neno lake Mungu ambalo li hai, tena ni kweli.
HESABU 23:19
Mungu si mtu, aseme uongo.
Mungu ni Mungu Mwenyezi, yeye anaweza mambo yote isipokuwa kusema uongo, naye asema hivi
MARKO 11:24= kwasababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali aminini yakwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Katika somo litakalofuata nitafundisha kuhusu Amani,
MUNGU AKUBARIKI
No comments:
Post a Comment