Wednesday, October 23, 2013
TOFAUTI KATI YA SERIKALI YA MBINGUNI NA DUNIANI
Na Mwijilisti Gerald Robert
Ufalme wa Mungu ni Serikali halisi iliyoanzishwa na Mungu (YEHOVA)
Katika Biblia serikali ya mbinguni huitwa Ufalme wa Mbinguni ni kwasababu inatawala kutoka mbinguni (Mathayo 4:17, na Marko 11:14-15)
Ufalme huo wa mbinguni kwa njia furani hufanana na serikari za kidunia, lakini Ufalme huo ni bora kuliko serikali za kidunia.
WATAWALA
Mungu alimchagua Yesu Kristo (Nafsi ya pili ya Mungu =Mungu Mwana) kuwa Mfalme wa Ufalme huo, na akampa mamlaka makubwa kuliko mtawala yeyote wa kibinadamu katika dunia hii (Mithali 28:18)
Yesu Kristo anatumia Nguvu hizo vizuri kwakuwa tayari amedhihirika kuwa ni kiongozi mwenye kutegemeka na mwenye huruma kuliko kuliko watawala wa kibinadamu (Mathayo 4:23) (Luka 7:11-17) (Marko 11:40-41 na 6;31-34)
Chini ya Mwongozo wa Mungu Baba , Yesu amechagua watu kutoka mataifa yote ambao watatawala wakiwa Wafalme pamoja naye huko mbinguni (Ufunuo 5:9-10)
MUDA
Tofauti na serikari za wanadamu ambazo hutawa kwa mtindo wa kubadilishana Ungozi kulingana na muda maalumu waliojiwekea na kukubaliana, au Wakati mwingine mtawala anapokufa huchaguliwa mtu mwingine kutawala,
Lakini kwa habari ya utawala wa mbinguni, yeye atawalaye hutawala milele yote , yaani utawala wake ni wakudumu na wala utawala huo hauta haribiwa kamwe (Danieli 21:44)
URAIA
Mtu yeyote anayefanya au kutimiza yaliyo mapenzi ya Mungu, mtu huyo ndiye anaweza kuwa Raia wa Ufalme huo wa Mbinguni, (Ufalme usio haribika) bila ya kujali Ukoo wake, Dini yake, Dhehebu lake, au Mahali alipo zaliwa, ilimladi tu atimize mapenzi ya Mungu (Matendo 10:34-35-35)
SHERIA
Sheria au Amri za Ufalme wa Mbinguni zinatimiza mambo mengi zaidi ya kukataza tabia mbaya, pia zinasaidia Raia wake kuwa wenye maadili mema
Mfano-: Biblia inasema ni lazima umpende Mungu (YEHOVA) kwa Moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa Akili zako zote. Hii ndio Amri iliyo kuu na yakwanza.
Yapili inayofanana na hii ni Umpende jirani yako kama nafsi yako (Mathayo 22:37-39)
kumpenda Mungu na jirani kunawafanya Raia wa Ufalme huo wafanye mambo yanayo wanufaisha wengine.
ELIMU
Ingawa ufalme wa mbinguni unawawekea raia wake viwango vya juu , lakini bado unawafundisha jinsi ya kutenda kulingana na viwango hivyo (Isaya 48:17-18)
MALENGO
Ufalme wa mbinguni huwa hauwanufaishi watawala wake huku ukiwakandamiza raia wake kama zilivyo serikali za kidunia, badala yake unatimiza mapenzi ya Mungu Baba, na huku ukiwahaidia raia wake (yaani wale wanaotimiza mapenzi ya Mungu) Uzima wa Milele katika Dunia ya paradiso ( Ufunuo 21:1-4) (Isaya 35:1-6) (Mathayo 6:10)
. . .MUNGU AKUBARIKI, JIANDAE KWA SOMO LINALOFUATA. Amen. . .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment