Wednesday, October 23, 2013

KANISA LA VAMIWA MWANZA



Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia tarehe 21october 2013 ndani ya kanisa la Gilgal Christian Worship Centre Pasiansi, Ilemela Mwanza.

Tukio limetokea saa saba usiku ambapo Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi pia na mwenyekiti wa vijana wa kanisa aliuwawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine ambapo Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu walijeruhiwa na hali zao sio nzuri lakini wako Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kutokana na mapanga waliyokatwa.
Askofu wa kanisa Eliabu Sentoz alisema kama Jeshi la Polisi likiamua kukomesha hivi vitendo inawezekana kuvimaliza kabisa ambapo kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ernest Mangu amethibitisha tukio limetokea
lakini mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa kitu ambacho kinaongeza maswali zaidi kuhusu tukio lenyewe.


.


Wananchi nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre Pasiansi Ilemela Mwanza.


Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza.
Mabaki ya Dmu katika Eneo la Kanisa

Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.

INJILI FOREVER INAWAPA POLE VIONGOZI WOTE WA KANISA
Source: Dj Sek Blog

No comments:

Post a Comment