Wednesday, October 16, 2013

PIERRE NKURUNZINZA: RAISI ALIYEOKOKA AFRIKA MASHARIKI

PIERRE NKURUNZINZA

Rais wa Burundi aliye okoka na muimba sifa kanisani.
                                         
       Pierre Nkurunzinza  amezaliwa 18/12/1963 akiwa ni mtoto wa Mwanasiasa Eustache Ngabisha, Eustache Ngabisha aliwahi kuwa mbunge katika bunge la Burundi 1965 pia kuwa Gavana wa majimbo mawili kabla ya kuuliwa mwaka 1972 kutokana na migogoro ya kikabila watutsi na wahutu mauaji ambayo yaliwaghalim watu 300,000 na wengine kukimbia kama wakimbizi katika nchi za jirani.

SABABU YA KUINGIA KATIKA SIASA

Akiwa mhadhili katika chuo kikuu cha Burundi 1995 jeshi la watutsi walikivamia kampas ya chuo na kuua wanafunzi takribani 200. Anasema "1995 jeshi la kitutsi lilivamia kampas ya na kuua wanafunzi 200. Walijaribu kuniua kwa kupiga risasi gari langu lakini nilifanikiwa kutoka na kukimbia, waliliharibu sana gari langu baada ya hapo nikaamua kujiunga na CNDD-FDD kama mwanajeshi". Hio nukuu nimeitafsiri tafadhali ili watu wengi waelewe.
 Pierre Nkurunzinza alikuwa Raisi wa kwanza kuchaguliwa kwa demokrasia mwaka 2005 na kuchaguliwa tena kwa kishindo mwaka 2010 ambapo alishinda kwa kishindo 91% walimchagua kuwa Raisi. Raisi Nkurunzinza licha yakuwa anaimba kanisani kwake pia alishawahi kuonekana katika mahojiano maalum BBC SWAHILI.


Rais Pierre Nkurunzinza akimwabudu Mungu Kanisani.

LENGO LA KUANDIKA HISTORIA YA PIERRE NKURUNZINZA

Nikuwakumbusha Ndugu zangu walio amua kumkubali Bwana Yesu kuwa na ujasiri zaidi katika kujitangaza wameokoka kwani nakumbuka nilipokuwa shule ya msingi Chamwino Primary School(DODOMA) nilikuwa naona aibu sana kusema nimeokoka kwani ilikuwa baada ya hapo nikuchekwa utaokokaje bado mtoto?? basi nikajua labda ni utoto wao tu ndio maana wananicheka, nimeshangaa mpaka nimekuwa nimegundua hata wazee vijana, wazee wa kati, wazee kabisa nao huchekwa nakuonwa ni washamba.

       Pia nawasihi wale ambao hawajaokoka na Mungu amekuwa akisema nao kuhusu kuokoka ila wanaona aibu kwa kuchekwa na watu watambue kuwa maisha ya duniani ni mafupi sana na huko tuendako ndiko nyumbani. ulishawahi kujiuliza Nyumbani kwako patakuwa wapi?? Kama hujui jiulize maisha yako yanamuwakilisha nani hapa duniani??
      Binafsi nimegundua sio lika fulani ndio huwashangaa bali ni shetani huwaingia na kujaribu kukuvunja moyo. ila tambua Yesu uliyenaye ni mkuu sana. Nafurahi kuwaona wenyeviti wa serikali wa mitaa, madiwani, wabunge, Raisi wakiwa wameokoka kwanihuyafanya maisha yao na vyeo vyao kumtukuza Mungu.

IMEANDIKWA NA ROBERT MAZIKU

No comments:

Post a Comment