HII NI SIRI
By Apostle Eliya
YALIYOMO
1. UTANGULIZI
2. SIRI
3. HITIMISHO
LENGO LA SOMO
- Kufunua Siri iliyofichika
-Kuonyesha umuhimu wa kubadili vipaumbele vyetu
ANDIKO KUU ;- KOLOSAI 1:26 “Siri ile iliyofichwa tangu
zamani zote na tangu vizazi vyote,bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake”
1.UTANGULIZI
-Ninapoangalia mimea, wanyama, sayari, mazingira na ulimwengu kwaujumla ninagundua kwa hakika kuna kitu kinapungua, kuna siri imejificha.
-Hapa ninapoandika haya mafundisho kuna siri nyingi
zimenizunguka, hata hapo unaposoma haya mafundisho ya Apostle Eliya, kuna siri
nyingi zimekuzunguka. Hapo ulipo unaweza kuingia katika Bustani ya Edeni ambayo
Adam na Hawa walifukuzwa miaka 6000 iliyopita. Sasa twende wote tukagundue hii
siri……..
2. SIRI
- Najua watu wengi hawajui kilichotokea katika bustani ya Edeni wakati wa Adam na Hawa, wana Theolojia wamejaribu kutengenezea somo ailimradi watengeneze mtaala, lakini wameshindwa kufunua siri iliyokuwa imejificha. Hata hivyo Theolojia sii ya Muhimu sana. Asili ya Biblia ni Rohoni, ukiingia rohoni utaigundua, kwahiyo hatuwategemei wana theolojia kutuchambulia kila kitu, Hapana.—2 Petro 1:21
a).Bustani ya Edeni – NWANZO 2:8-9
- Bustani ya Edeni ni bustani ambayo ndani yake kulikuwa na
bustani nyingine ndogo.
- Kinachofanya wapendwa wengi wasielewe hizi sura za mwanzo
kwasababu hizi sura za mwanzo zinachanganya matukio ya kimwili na kiroho. Mungu
aliumba Dunia na vitu vyote kwa siku sita, siku ya saba akapumzika, cha ajabu
siku hii ya pumnziko ndo aliamua apande bustani. Hii bustani ilikuwa niya
kiroho na vyote vilivyochipushwa vilikuwa ni alama za rohoni.
- Kitu cha muhimu katika hadithi ya Bustani ya Edeni ni miti
iliyokuwa imepandwa, kulikuwa na miti mitatu ; 1. Mti unaotamanika kwa macho na
unaofaa kuliwa, 2. Mti wa uzima na 3.Mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Miti hii
mitatu pamoja na matunda yake yote niya kiroho. Mungu aliwaambie matunda ya mti
wa kwanza na wapili wanaruhusiwa kula ila matunda ya mti wa tatu hawakuruhusiwa
kula.
-Mti wa Kwanza ni Roho
Mtakatifu, na mti wa pili ni Yesu na mti wa tatu Shetani. Hii bustani ambayo ni
mbingu ya pili tulipewa wanadamu kuimiliki, kwahiyo Dunia pamoja na mbingu ya
pili(ulimwengu wa kiroho) ilikuwa ni mali ya Adam na Hawa, kwa kule kuasi kwao
wakapoteza haki ya kumiliki ulimwengu wa kiroho pamoja na huu ulimwengu, vyote
vikawa chini ya Shetani, lakini ile bustani ndogo ndani ya Edeni haikuwa chini
ya Shetani kwasababu ilifungwa, ingawa ipo ndani ya Edeni.
b).Adam na Hawa
- Waliumbwa katika ulimwengu huu wa mwili – Mwanzo 2:7
Pumnzi aliwapulizia ilikuwa ni Uhai(uwepo wa Mungu),
namaanisha Roho Mt,hii Roho ilitoka baada ya uasi na ilirudi rasmi wakati wa
Yesu—Yohana 20:22, ndio maana waliweza kuwekwa katika ulimwengu wa
kiroho(Edeni), shetani alimuingia nyoka akamdanganya Hawa na hatimaye Adam
akashawishika. Matokeo walifukuzwa nnje toka Bustani ya ndani ya Edeni, na pia
walifukuzwa ndani ya Edeni, yale makalipio aliyoyatoa Mungu yalikuwa katika
ulimwengu wa kimwili. Mwanzo 3:16-19
-Kwanini walifukuzwa ?
Tayari walishafanya Dhambi kilichotakiwa kufuata ni kutubu
na mwisho kula matunda ya ile miti miwili, lakini hiyo toba haikutakiwa
ifanyike kwa mdomo, hapana, lilitakiwa jambo lifanyike katika ulimwengu wa
kimwili, lazima damu imwagike. Sasa mwanadamu hakujua kuwa amefanya kosa ambalo
lina GHARAMA NYINGI na KUBWA za kulipa. Unadhani walikula vipi tunda ?
c).Kurudi Tena katika Bustani ya Edeni.
- Kikwazo cha Adam na Hawa cha kutokuruhusiwa kuingia tena
katika Bustani ya Edeni ni Dhambi ambayo malipo yake hakuna mwanadamu ambaye angeweza
kulipa, sasa Yesu ameshalipa, nini kilichobaki ? Kumbe hapo ulipo unaweza
kuingia tena katika Bustani ya Edeni, najua huwezi kuamini lakini kile kikwazo
kimeondolewa. Kuingia tena katika ulimwengu wa kiroho ni haki yako, hapo ulipo
upo karibu sana
na Bustani ya Edeni, tatizo ni nini ? umefumbwa macho – Efeso 1:18
d).Umuhimu wa Kuingia Bustani ya Edeni.
- Siri za kila mwanadamu unaweza ukazigundua kama utaingia bustani ya Edeni, manabii wote Mungu
aliwapa neema ya kuingia katika ulimwengu wa kiroho bila wale Malaika walinzi
kuwasumbua – Ezekieli 37:1-2. Henoki alitumia Muda wake mwingi kuwa katika
Bustani ya Edeni ndio maana Mungu akamwambia baki hukuhuku—Mwa 5:24, vipi
kuhusu Nabii Eliya Mtishibi ?—2 Wafalme 2:11, wote hawa wapo katika Edeni
wanakula good-time. Mtume Paulo aliweza kuperuzi ulimwengu wa kiroho, Stefano
wakati wanampiga mawe aliweza kuperuzi ulimwengu wa kiroho – Mdo 7:55, Yesu
aliwaambia wananfunzi wake nilimuona shetani akianguka toka juu, wewe unadhani
Yesu alimuonaje shetani pasipokuwa alikuwa katika ulimwengu wa kiroho ? Watu
wengi unaowasoma katika Biblia waliweza kuingia katika ulimwengu wa kiroho na
kurudi katika ulimwengu wa kimwili, nikama vile kufumba na kufumbua macho.—Marko
9:4
- Huu ulimwengu
tunaouishi, haukutengenezwa ilitujifunze mambo yaliyomo, HAPANA, tulipaswa kuwa
tunajua mambo yote bila kufundishwa kwasababu siri zote zimefichwa katika
Edeni. Ndiyo maana mimi nasema huu mpango wa shule sio kwa ajili
yakukuelimisha, bali kukupotezea muda ili usijue unapotakiwa kuwepo. Huu
ulimwengu na mambo yote yaliyomo ni rahisi kuyafahamu ukiwa rohoni, lakini
ukiwa mwilini itakughalimu sana,
kwasababu haukutengenezwa kwa mtu wa mwilini, ndio maana uchunguzi mmoja wa
kisayansi unaweza ukachukua muda mwingi na mapesa mengi. Ngoja nikuulize,
mfalme dawa ya kumtibu mfalme Hezekia, nabii Isaya aliisomea wapi ?
-Ngoja nikushitue kidogo ; Wanasayansi wanasema kipenyo cha Ulimwengu
ni Maili 93 bilioni, ukipita katikati ya hiki kipenyo kwa mwendo kasi wa mwanga
itakuchukua miaka 28 Bilioni kumaliza kipenyo cha ulimwengu, unajifunza nini
hapa? Kama umefunguka kimawazo utagundua mambo
yanayoendelea ulimwenguni ni juu ya akili za asili za mwanadamu wa kawaida.
Kila mbegu unayoiona imetengenezwa kwa namna ya ajabu na huwezi kugundua kwa
macho yako viwango wa kabohaidreti, protini, fati na nguvu iliyomo ndani ya
kila mbegu, na kuichunguza mbegu moja inaweza ikakugharimu muda na gharama,sasa
kuna mbegu mabilioni. Vipepeo unaowaona wapo aina chungu nzima, hujaingia
kwenye miti na matunda pamoja na elimu ya unajimu. Ngoja nikwambie, kuna
Galaksi Mabilioni katika huu ulimwengu wetu, kila galaksi ina nyota karibia
Bilioni 100. Hii Dunia yetu ikiingizwa ndani ya jua, zitatakiwa Dunia karibia
Milioni moja ili upate ukubwa wa Jua, umbali wa kutoka hapo ulipokaa mpaka
kwenye Jua ni mabilioni ya maili.
Kwavipimo hivi, nani aliumbiwa huu ulimwengu ? hata akili zetu haziwezi
kufikiri ? ndomaana nikasema kuna siri imefichika.
- Waulimwengu
Waulimwengu ni watumishi wa shetani wanaofanyakazi kwa jina la
serikali, makampuni, viwanda, taasisi, mashirika. Amini au usiamini shetani
anajua ule uwezo ambao Mungu alituumbia na tukaaupoteza na kisha akaturudishia
tena, hataki tutambue haya mambo ndiomaana anajaribu kutupotezea muda kwa
mtindo wa AJIRA, ajira ni kifungo kimojawapo kizuri sana, Mchakato wa elimu
pamoja na mitaala yake pia ni kifungo. Daktari mmoja alisema alichukua miaka 40
kumchunguza nyani,hebu ona !! huku sinikupoteza muda !!, haya ndio madhara
tunayoyapata kwa ile dhambi ya asili na kukataa kuingia katika bustani ya Edeni.
Fanya urudi Bustanini. Ndio maana ukisoma Biblia vizuri hukuti hata sehemu moja
Mungu akiwaambie Waizraeli sumbukieni maisha, anajua nini tulichokipoteza na
hakirudi kwa kufanya majaribio mengi ya kisayansi, siku zote aliwaambia mkitii
mtakuwa watu bora Duniani. Tatizo liko rohoni.—TORAT 7:14
e).Mapepo katika ulimwengu wa kiroho.
-Malaika walioasi wote walitupwa kuzimu, lakini muhura wao
bado haujafika wa kufungwa kwahiyo wanatumia muda mwingi kuwa katika ulimwengu
wetu na ule tulioupoteza wa kiroho, mipango mingi hupangwa huko, wala hatuoni
ndio maana wanatutesa. Kama tungekuwa na uwezo wa kurudi Bustanini, tungeweza
kufukuzana nao na kuwakamata na kuwapiga kwasababu mwendokasi wao sio mkali
ukilinganisha na mwendokasi wetu wa mawazo, kama roho zetu zingeweza kuingia
ulimwengu wa kiroho tungeweza kutoka sayari moja na kwenda nyingine kwa
sekunde, kama Pepo limejificha nyuma ya sayari ya Pluto ningeweza kwenda mara
moja na kumkamata na kumtupa kuzimu tena. Kumbuka Edeni alipewa Mwanadamu sio
Shetani.
-Kwakweli tulipoteza kitu cha muhimu sana, macho yetu ya kiroho yalifungwa. Mpaka
muda huu ninaoongea wanadamu hawajui umuhimu wa kurudi tena katika Bustani ya
Edeni, tumeshazoelea shida, ndio maana hatuogopi kufanya dhambi, kumbe kila
dhambi tunayoifanya inatufumba macho ya kiroho, watoto wadogo wanahuo uwezo
kuingia katika Bustani nzuri ya Edeni lakini anapokuwa na kuanza kufanya dhambi
macho yake yanafumbwa, maana yake anafukuzwa katika bustani,sasa kurudi tena
nikasheshe.
3.HITIMISHO
-Kama hujakubaliana na mimi, fanya uchunguzi wa kila kitu
duniani, kama utashindwa haimaanishi wewe huna akili au muda wako wa maisha ni
mafupi, HAPANA, badala yak e nikwamba ulimwengu huu wa mwili uliumbwa kwa ajili
ya mtu wa kiroho. Ugumu upo kwasababu tunataka tuugundue kwa namna ya kimwili.
-Vitabu vya siri za huu ulimwengu viliachwa katika bustani
ya Edeni, tafadhari turudi tukasome tufurahie maisha. Lakini, tutaingiaje
Bustanini wakati kuna Malaika walinzi ?—Mwanzo 3:24.
……………….….THE BEST HAS COME…………………